-Awapotosha waTanzania ili wasije kuongea na Rais Kikwete
-Amdanganya Rais Kikwete darasa la Kiswahili lipo “Summer Break”
-Mh. Kikwete amwambia Idd Sandaly “YOU ARE ON YOUR OWN”
“Team Libe for DMV Community President 2014” inatoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaniza Mh. Jakakya Mrisho Kikwete kwa kutumia muda wake wa thamani na kukutana na waTanzania hapa DMV. Zaidi, tunapenda kutoa pongezi nyingi kwa mama Balozi Liberata Mulamula na wafanyakazi wa ubalozi kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na watanzania wa hapa Marekani siku ya Jumamosi August 2, 2014. “Team Libe for DMV Communoty President 2014” tunasema asante!
Baada ya kumaliza kutoa shukrani za dhati kwa Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi, Liberatus Mulamula; “Team Libe for DMV Community 2014” tunaamini kuwa tuna wajibu wa kutoa mrejesho juu ya kilichojili kwenye mkutano na Rais. Tutaanza kutoa mrejesho juu ya upotoshaji uliotawala kwenye zoezi zima la kuongea na Mh. Rais. Zoezi hili liliongozwa na Rais wa DMV aliye maliza muda wake Ndg. Idd Sandaly kwa kufanya upotoshaji ufuatao;
Upostoshaji wa kwanza ulio fanywa na Idd Sandaly ni
kuwa; watu wote walio taka kuja kuongea/kumuona Rais, Jakaya Kikwete, iliwapasa waje na ID au Passport. Upotoshaji huu ulikuwa umewekwa ili kuwawanyima haki waTanzania wasio na ID au wametokea kupoteza passport kwa bahati mbaya. Ukweli ni kuwa; kwenye kumuona Mh. Rais kulikuwa hakuna maswala ya kuonyesha ID wala passport. Watu waliingia bila kuonyesha hivyo vitambulisho.
kuwa; watu wote walio taka kuja kuongea/kumuona Rais, Jakaya Kikwete, iliwapasa waje na ID au Passport. Upotoshaji huu ulikuwa umewekwa ili kuwawanyima haki waTanzania wasio na ID au wametokea kupoteza passport kwa bahati mbaya. Ukweli ni kuwa; kwenye kumuona Mh. Rais kulikuwa hakuna maswala ya kuonyesha ID wala passport. Watu waliingia bila kuonyesha hivyo vitambulisho.
Upotoshaji wa pili ulio fanywa na Ndg. Idd Sandaly ili awezi kuwanyima waTanznia haki ya kukutana na Rais wetu ni kuwa; Idd alitoa maelekezo kuwa mkutano na Rais utaanza saa 12 jioni (6pm) na watu wanatakiwa kuwa pale saa 11:40 (5:40pm) na endapo usipo kuwapo pale kwenye huu muda, hautaruhusiwa kuingia. Ukweli ni kuwa, mkutano ulianza saa 1:30’s (7:30’s pm), na watu walikuwa wanaingia muda wowote. Huu upotoshaji umewasababishia watu wengi kuto kuja au kupoteza masaa yao ya kazi na shughuri zingine.
Upotoshaji mwingine ulio fanywa na Idd Sandaly ni kuwa; alikuwa akitoa taarifa kuwa watu wanao takiwa kuingia ni 250 na hakuna mtu atakaye ongezwa kwenye “roaster” endapo asipo rudisha jina lake kabla ya Ijumaa saa sita mchana. Ukweli ni kuwa; kulikuwa na watu zaidi ya 300 na wengine walikosa viti. Sio hilo tu, wapo wale ambao waliandikishwa baada ya saa sita mchana Ijumaa, kitu ambacho si haki kwa wale walio tiwa upofu na upotoshaji huu. Huu upotoshaji unatukumbusha kilicho tokea December 2013 “Uhuru Day” ambapo Idd Sandaly akishirikiana na Vijimambo blog aliweza kuwa “rip off” wana DMV $60.00 na kuwapeleka kwenye Godauni ambalo lilikuwa na vumbi, hakukuwa na security, na pombe ilitolewa mbele ya watoto. Hii ilikuwa siku ambayo Mh.January Makamba alikuja DMV.
Upotoshaji mwingine wa Idd Sandaly ni kuwa alitumia mkutano wa Mh. Rais Jakaya Kikwete na waTanzania kama sehemu ya kufanyia kampeni. Hii ilidhihirika pale ambapo Idd Sandaly alipo jipigia debe mbele ya kadamnasi na kusema “uchaguzi Jumamosi naomba mnipigie kura”. Busara za Mheshimiwa Kikwete zilitamaraki na kumjibu kwa kumruka akasema “ YOU ARE ON YOUR OWN”.
Upotoshaji wa mwisho ambao ni hatari kwa taifa ni Idd Sandaly kuongea UONGO mbele ya Rais. Ndg Idd Sandaly amemdaganya Mh. Rais Jakaya Kikwete, balozi Liberata Mulamula, Waziri Bernad Membe, waziri Magufuli, naibu waziri wa nishati Mh. Stephene Masele na waTanzaia wote walio kuwepo kwenye mkutano na Rais jana kuwa DARASA LA KISWAHILI LIPO na watoto wapo “Summer BREAK”. Huu ni UONGO ambao unaonyesha Idd Sandly ni kiongozi wa aina gani kwa kuwadanganya watanzania na Mh. Rais Jakaya Kikwete. Kiongozi anaye danganya umma hana maadili wala dhamana ya kuongoza. UONGO wa Idd Sandaly kuwa darasa la Kiswahili lipo “Summer break” unathibitika kwa sababu zifuatazo: Mosi, hakuweza kusema hiyo “Summer Break” itaisha lini (ni ya muda gani), pili hakuweza kutoa anuani ya darasa (darasa lipo wapi) na tatu darasa lime kufa kabla ya February 2014; hatuna uhakika kama “Summer Break” ya darasa hili huanza February!
Mwanaid Love “Mona”
Campaign Manager
Team Libe for DMV Community President 2014