Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mhe: Athuman Mwenda akipata maelezo ya kina jinsi ya uandaaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wakulima ili kufanikisha kauli mbiu ya mwaka huu yenye ujumbe wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’-Kilimo ni Biashara, vilevile Mamlaka inatekeleza mkakati wa Taifa wa KILIMO KWANZA.Maelezo hayo yalikuwa yakitolewa na kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi Dkt. Ladislaus Chang’a katika banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa kwenye maonesho ya NaneNane 2014, viwanja vya Nzuguni-Dodoma
No comments:
Post a Comment