ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 16, 2014

AFANDE SUZAN KAGANDA APOKEA ASKARI WAPYA 75 TABORA, ATOA TAARIFA YA UHALIFU MKOANI HUMO

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya Polisi. Kamanda aliwataka askari hao kufanya kazi kwa weledi katika utendaji kazi pamoja na Nidhamu ya hali ya juu. 
Askari wapya wakimsikiliza Afande Suzan Kaganda alipowapokea mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 16/09/2014.

Ndugu waandishi wa habari katika mkoa wetu wa Tabora kumetokea matukio yafuatayo:-

KUPATIKANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA NA PIKIPIKI ZA WIZI: Huko wilaya ya Igunga wamekamatwa watuhumiwa watatu:-
1. WILLY
s/o MASHILINGI, 22 yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Kahama.
2. SITA
s/o JILUNGA, 38 yrs, msukuma, mkulima na mkazi wa Nzega.
3. YUSUPH
s/o MIHAYO, 24yrs, msukuma, mkulima wa mtaa wa Stoo.
4. GILALA
s/o BULEBA, 35yrs, msukuma, mkulima, mkazi wa Igunga mjini.

wakiwa na madawa ya kulevya wanayoyatumiwa kulewesha watu kisha kuwapora pikipiki. Walipohojiwa walikiri kuhusika na matukio mbali mbali ya wizi wa pikipiki na kuonesha pikipiki mbili zenye namba T 892 CXB, T 522 CQZ, T.914 BUW na T.812 CGU zote aina ya SANLG ambazo walizipora huko Puge wilaya
ya Nzega. Juhudi za kuwatafuta wamiliki halari wa pikipiki hizo zinaendelea.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

KUPATIKANA NA BHANGI GUNIA MBILI:
Huko wilaya ya Nzega amekamatwa mtuhumiwa MABULA s/o EZEKIEL, 23yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Ibologero akiwa na bhangi gunia mbili. Mtuhumiwa baada ya mahojiano amekiri kuwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

AJALI YA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU NA KUSABABISHA VIFO:
Huko kijiji cha Ndono barabara ya Urambo gari no. T607 BNV scania lorry iliyokuwa ikiendeshwa na FUMBA s/o JUMA, 45yrs, Msambaa, mkazi wa DSM iligongana na pikipiki ya kubeba mizigo (Guta) REG no.

T153 CWJ SUNLG na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo ambao ni MAHONA S/O MUSA WANDEZI, 30yrs, Msukuma, mkazi wa Intika dereva wa pikipiki, HIBHA S/O LUCAS, 30yrs, msukuma, mkazi wa Ndono, MABULA S/O MATONGO, 35yrs, msukuma, mkazi wa Intika chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki.

AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO:
Huko maeneo ya barabara kuu Nzega – Igunga katika kijiji cha Kitangili GARI T.300 CWB Toyota Hiace ikiendeshwa na STANSLAUS S/O JOAKIM, 33yrs, Mchaga, mkazi wa Nzega ilimgonga mtembea kwa miguu JOKU D/O MBEGESHEN, 32yrs, Msukuma, M/biashara, mkazi wa Singida na kufa papo hapo.

Chanzo cha ajali ni uzembe wa mtembea kwa miguu kuvuka barabara bila tahadhali. Dereva amekamatwa kwa mahojiano zaidi.

Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua wahalifu, pia watumiaji wa barabara wafuate sheria za usalama barabarani.
CREDIT:GPL

No comments: