Friday, September 12, 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA MAZUNGUZO NA BALOZI MPYA WA JAPANA PAMOJA NA UJUMBE WAKE TOKA KAMPUNI YA TEHAMA YA NEC LEO JIJINI DAR ES SALAM

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil( Meza Kuu) akiongoza mazungumzo rasmi na Balozi Mpya wa Japani nchini Tanzani(haonekani katika picha) alipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo Septemba 12, 2014( wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Haji Janabi.
Balozi Mpya wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Balozi Masaki Okada(wa pili kushoto) akiwa pamoja na Ujumbe wake toka Kampuni ya Kijapan ya NEC inayojishughulisha na Mifumo ya Kiusalama ya TEHAMA.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) akifuatilia kwa makini mazungumzo rasmi ya Balozi mpya wa Japani
nchini Tanzania(hayupo pichani). Wengine kushoto ni Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia mazungumzo hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil( Meza Kuu) akiongoza mazungumzo rasmi na Balozi Mpya wa Japani nchini Tanzani(haonekani katika picha) alipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo Septemba 12, 2014 akiwa na ujumbe wake toka Kampuni ya Kijapani ya NEC inayojishughulisha na Mifumo ya Kiusalama ya TEHAMA.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil( wa pili kushoto) akiwa ameketi katika picha ya pamoja na Balozi Mpya wa Japani nchini Tanzani, Mhe. Balozi. Masaki Okada(wa pili kulia). Katikati ni Rais wa Kampuni ya Kijapani ya NEC inayojishughulisha na Mifumo ya Kiusalama, Dkt. Nobuhiro Endo.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(kushoto) baada ya mazungumzo rasmi na Balozi Mpya wa Japani nchini Tanzania akiwa na Ujumbe wake leo Septemba 12, 2014 Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake