ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 14, 2014

SHUKURANI KUTOKA KAMATI YA VIJIMAMBO.

Kamati ya Vijimambo inependa kutoa shukurani zake za dhati kwa wadau wake wote waliofika katika tamasha la utalii na miaka 4 ya Blog ya Vijimambo. Sisi wanakamati pamoja na timu nzima ya Vijimambo tumefarijika sana kuona wadau mbalimbali wa Vijimambo waliokuja kutoka kila kona ya Dunia na kujumuika nasi tangia asubuhi na usiku bila kuchoka.

Shukurani za pekee zimuendee Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu kwa kukubali mwaliko wetu wa Blog ya Vijimambo na kukubali kuungana na sisi na kushereheka nasi tangia mwanzo mpaka mwisho. 

Shukurani zetu kwa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwani yeye alitambua umuhimu wa tamasha hili tangia mwanzo na kukubali kushirikiana nasi tangia siku ya kwanza tulipo mpelekea mawazo na nia yetu ya kusherehekea miak 4 ya Vijimambo kwa kutangaza utalii wa Tanzania na kukemea ujangili unaojaribu kutokomeza na kuangamiza vivutio vya Ualii ambao ni kipato moja wapo muhimu kwa Taifa letu linaloendelea.

Shukurani kwa Immaculata Diyamet wa kitengo cha Utalii Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Afisa Suleiman Saleh kwa mchango wao na mawazo yao yalioboresha Tamasha hili kwa asilimia zote uwepo wenu umesaidia sana tunasema asante sana.

Shukurani za pekee kwa Wajasiliamali waliosshirikiana bega kwa bega na Vijimambo katika kufanikisha siku hii muhimu katika historia ya Bog ya Vijimambo. Ni kitu cha kujivunia kwa blog ya Vijimambo kwa ushirikiano wa karibu inaopata na wajasiliamali mbalimbali wa Marekani na kwingineko Duniani, kwa ushirikiano wenu na kufanyakazi kwa karibu na Blog ya Vijimambo kumewezesha kufanikisha Tamasha hili na kutuwezesha kutoka kifua mbele na kuthubutu kusema TAMASHA LILIKUA LA MAFANIKIO.

Asante na kwa mapenzi yake Mola tutaonana mwakani.

Mwenyekiti wa Kamati
Baraka Daudi

No comments: