Wednesday, September 17, 2014

UNCDF KUENDELEA KUSAIDIA KUJENGA UWEZO WA KIFEDHA KUHUDUMIA MAENDELEO

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa, akizungumza kwenye mkutano wa watendaji waandamizi wa serikali kutoka katika Ofisi ya WaziriMkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) pamoja na waandishi wa habari kuhusiana na Programu ya Utafutaji Fedha Nchini kwa maendeleo ya wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI) ambayo ilianza katika awamu ya majaribio 2012 na kuonyesha mafanikio. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Ufundi wa programu hiyo nchini Tanzania , Peter Malika.

Na Mwandishi wetu

Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) umefurahishwa na programu zinazoendeshwa nchini kwa msaada wake na kusema upo tayari kuendelea kufanyakazi na serikali na wananchi wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa katika ziara ya Katibu Mtendaji wa UNCDF, Judith Karl, ambaye anaitembelea Tanzania kwenye mkutano wake na watendaji waandamizi wa serikali kutoka katika Ofisi ya WaziriMkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) jana.

Karl ambaye ameongozana na Mkurugenzi wa Local Development Finance kutoka Makao Makuu ya UNCDF, New York, David Jackson alisema wamefurahishwa namna Tanzania inavyotekeleza mpango huo wa kuwezesha watanzania kuchangia miradi yao ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya ndani katika halmashauri mbalimbali.Miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema ni Same na Kibaha.

Akiwa na Mshauri Mkuu wa Ufundi wa programu hiyo nchini Tanzania , Peter Malika, Mtendaji huyo alisema wamefika kutia saini mkataba wa maelewano kati ya Tanzania na shirika hilo la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kutekeleza miradi 25 na hasa baada ya awamu ya kwanza wa miradi mitano kuonesha mafanikio makubwa.

Akizungumza Karl pamoja na kuelezea kazi za UNCDF nchini Tanzania alitangaza kuanzishwa kwa Programu ya Utafutaji Fedha Nchini kwa maendeleo ya wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI) kwa mwaka 2014-2017, ikiwa ni jitihada mpya ya UNCDF iliyoanzishwa kufuatia maarifa yaliyopatikana katika utekelezaji wa LFI ya kwanza (Tanzania) katika awamu ya majaribio (2012-2015).
Katibu Mtendaji mpya wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), Bi Judith Karl akizungumza na baadhi ya wajumbe wa TAMISEMI pamoja na waandishi wa habari juu Programu ya utafutaji fedha nchini kwa maendeleo ya wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI), ambapo alitangaza kuizindua rasmi program hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu – OWM-TAMISEMI, Dkt. Deogratius Mtasiwa.

Hadi sasa, programu ya majaribio ya LFI nchini Tanzania inasaidia miradi 25 ya miundombinu iliyoanzishwa na wawekezaji wa umma na binafsi na ambayo iko katika hatua mbalimbali za uendelezaji. Lengo la programu hiyo ni kuanzisha makampuni makubwa ya uwekezaji katika halmashauri ili kupunguza mchango wa serikali kuu katika mambo ambayo yanaweza kufanywa na wananchi na wao wakabaki katika sera na mipango mikubwa.

Miradi imetawanyika katika sekta mbalimbali zikiwezo za usindikaji bidhaa za kilimo, nishati, miundombinu ya utoaji huduma za jamii, mawasiliano, na uzalishaji viwandani, katika mikoa 10 kote nchini.

Miradi mitano iliyopiga hatua kubwa zaidi inatarajiwa kufikia kikomo cha bajeti yake katika miezi sita hadi tisa ijayo ambapo dola milioni 26 za mtaji wa ndani katika muundo wa mkopo na misaada ipatayo dola milioni 3 ilihamasishwa.

Msaada wa LFI kwa miradi ambayo iko katika muundo wa utaalamu wa kiufundi, kutoa amana, misaada ya kifedha , mikopo ambayo inahitajika sana kwa miradi midogo na ya kati ya miundombinu ili ivutie uwekezaji.

Matokeo ya jumla ya LFI ni kuongezeka kwa ufanisi wa rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya hapa nchini kupitia uhamasishaji kwanza kabisa wa mtaji binafsi kutoka nchini na masoko ya mitaji ilikuwezesha na kuhamasisha maendeleo ya mahali yaliyojumuishi na endelevu.
Mshauri Mkuu wa Ufundi wa programu hiyo nchini Tanzania , Peter Malika, Mtendaji akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo alisema kuwa lengo lake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, fedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini-TAMISEMI, Rebecca Kwandu na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa.

Katika mauzungumzo hayo ambapo Naibu Katibu Mkuu – OWM-TAMISEMI, Dk Deogratius Mtasiwa alikuwepo, UNCDF imesema inatambua ushirikiano mzuri kabisa uliotolewa na serikali kupitia OWM-TAMISEMI, hasa wajibu wake kama mshirika katika utekelezaji wa programuya LFI na kusaidia kubaini na kuendeleza miradi ya miundombinu inayofaa kwa biashara inayofadhiliwa na mamlaka za serikali za mitaa.

Katika ziara yake Katibu Mtendaji huyo anatarajia kuona namna ya kupanua msaada wa UNDCF kwa Tanzania.

Misaada hiyo ni pamoja na uanzishwaji wa huduma bunifu inayosaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za fedha na kujaribu njia za kufungua milango ya mtaji wa mahali ili kuwekeza katika miradi ya maendeleo.

Shabaha ya UNDCF ya kutoa mtaji wa uwekezaji na utaalamu wa kiufundi kwa sekta ya umma na ya binafsi umelenga kuwezesha mikopo na uazimaji fedha wa ngazi ya juu na utaalamu wa kiufundi katika kuandaa maandiko endelevu na yenye manufaa ya kujenga uwezo na miradi ya miundombinu.

Aidha UNCDF inaelekeza jitihada zake katika kuimarisha menejimenti ya masuala ya fedha za umma na mapato ya mahali, kuimarisha ubora wa uwekezaji wa umma na binafsi katika ngazi ya mahali.
Mkurugenzi wa Local Development Finance kutoka Makao Makuu ya UNCDF, New York, David Jackson akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo alisema wamefurahishwa namna Tanzania inavyotekeleza mpango huo wa kuwezesha watanzania kuchangia miradi yao ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya ndani katika halmashauri mbalimbali. Kulia ni Katibu Mtendaji mpya wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), Bi Judith Karl.

Kazi ya UNCDF katika masuala ya fedha jumuishi inalenga kuendeleza mifumo ya fedha iliyo jumuishi na kuahakikisha kuwa bidhaa mbalimbali za fedha zinapatikana katika matabaka yote ya jamii, kwa gharama nafuu, na kwa namna iliyo endelevu.

Lengo la asili la UNCDF – kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea – linaendelea kuwa na maana hata leo.

UNCDF wanaangalia ukuaji wa kiuchumi kama kitu muhimu katika kuongeza ubora wa maisha, kupunguza umaskini na kuendana na idadi ya watu inayozidi kukua.
Baadhi ya maafisa kutoka Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mtendaji mpya wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), Bi Judith Karl akipogezana na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa baada ya kuzinduliwa rasmi kwa program hiyo nchini. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini-TAMISEMI, Rebecca Kwandu na kushoto ni Mkurugenzi wa Local Development Finance kutoka Makao Makuu ya UNCDF, New York, David Jackson.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na Imanuel Muro kutoka UNCDF pamoja na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini-TAMISEMI, Rebecca Kwandu (katikati) mara baaada ya kumalizika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake