ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 21, 2014

WAREMBO MISS TANZANIA WASHUHUDIA UPIMAJI WAGONJWA WA EBOLA UWANJA WA NDEGE WA KIA

 Washiriki wa Shindano la Redd's Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Afisa Mfawidhi, Nisalile Mwangoka aliyekuwa akiwapa maelezo juu ya upimaji wa wageni wanao ingia nchini kupitia viwanja vya ndege unavyofanyika kutumia mashine maalum iitwayo 'Walk Through Thermoscaner', iliyopo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati warembo 30 wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea uwanja huo na kujifunza mambo mbalimbali . Warembo hao wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini. Mashine hiyo ikionekana kufungwa juu kuelekea usawa wa kuingilia abiria wanaowasili toka nje ya nchi.Namna inavyoonekana baada ya kipimo kuchukuliwa
 Nisalile Mwangoka akionesha kifaa cha zamani cha upimaji ugonjwa wa Ebola ambacho kimeelezwa kuwa licha ya ufanisi lakini kilikuwa kinaweka foleni kwa abiria tofauti na hicho kipya.Meneja wa Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Kisusi Makomondi akiwapa maelezo washiriki hao wa shindano la Miss Tanzaniua 2014 juu ya shughuli mbalimbali za uwanja huo. 
Warembo wakianza ziara. 
Camera man wa True Vision John Lymo akiwajibika uwanjani KIA.Warembo pia walipata fursa ya kutembelea kikosi cha zima moto uwanjani hapo.Warembo hao baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege KIA waliwasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Mkuu wa Wilaya (DC) wa Arumeru, Nyirembe Munassa Sabi,akiwa na warembo baada ya kuwapokea ambapo walitarajiwa kufanya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii hifadhi ya Arusha na Namanga katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

No comments: