Tuesday, September 16, 2014

Yanga ya Maximo haijaruhusu bao

Kocha wa Yanga Marcio Maximo.
Pia Yanga ikacheza na Thika United iliyokuwa nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya Kenya na kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa mfungaji akiwa Jaja. Rekodi hiyo iliendelezwa juzi Jumapili Uwanja wa Taifa kwa kuifunga Azam FC mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Hisani.
YANGA ikiwa chini ya Marcio Maximo imeweka rekodi ya kucheza mechi tano za kueleweka za kirafiki na kufunga mabao tisa bila ya kufungwa hata bao moja huku kocha huyo akisema inatokana na nguvu kazi waliyonayo.

Maximo ameliambia Mwanaspoti; “Kwanza ni timu nzuri ya benchi la ufundi, pili wachezaji wangu wanacheza kwa mtindo tofauti kulingana na ninavyotaka, mwisho kila mchezaji Yanga anatumika.”


Alisema anajisikia fahari kucheza mechi tano za ushindani bila kuruhusu hata bao moja kwani inaonekana anachofundisha kinafuatwa na wachezaji wake.


Yanga ikiwa kambini Pemba mwezi uliopita ilicheza mechi ya kwanza ya kirafiki chini ya Maximo dhidi ya timu ya daraja la kwanza ya Chipukizi na kushinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Gombani, mfungaji akiwa Genilson Santos ‘Jaja’.


Mechi ya pili ya Yanga ilikuwa dhidi ya Shangani ya daraja la kwanza Zanzibar kwenye Uwanja wa Amaan na kupata ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Andrey Coutinho na Salum Telela, pia ikacheza na bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, KMKM uwanjani hapo na kupata ushindi wa mabao 2-0 wafungaji wakiwa Coutinho na Hussein Javu.


Pia Yanga ikacheza na Thika United iliyokuwa nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya Kenya na kuifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa mfungaji akiwa Jaja. Rekodi hiyo iliendelezwa juzi Jumapili Uwanja wa Taifa kwa kuifunga Azam FC mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Hisani.


Kipa Deo Munishi ‘Dida’ ndiye aliyecheza mechi nyingi alisema: “Unajua kocha anatupa maelekezo muhimu kuhusu kuzuia kwani mimi kazi yangu ni kuwapanga mabeki na wote wananielewa japokuwa kuna wakati tunapotea kidogo.”


Naye beki wa kati na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema; “Mimi ndiye rais wa ulinzi Yanga na wenzangu tunaelewana na kutekeleza tunaloelekezwa na kocha, ndiyo maana hatufungwi hovyo. Kocha ananitumia kuelekeza wenzangu tangu Taifa Stars wakati ule.”


Safu ya ulinzi ya Yanga inaundwa na mabeki wa kati Cannavaro, Kelvin Yondani, mabeki wa pembeni Oscar Joshua (kushoto) na kulia Juma Abdul huku golini akiwa Dida. Pia Mbuyu Twite anacheza kama kiungo mkabaji.
Credit:Mwanaspoti

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake