Monday, October 27, 2014

ALICHOKISEMA RAY C KUHUSU KUKAMATWA KWA CHIDI BENZ NA MADAWA YA KULEVYA

“Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako,Mimi ni dada yako na
tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na
kutafuta suluhu,nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba
unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!!Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa
ya kulevya Inawezekana !!Watanzania
tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema
Tanzania Stand Up n Wish Him Luck With Love,Ray C Foundation.”

1 comment:

Anonymous said...

ray c chidi benz kaka yako akitoka rupangoni atakuja kukupiga tena na kirungu chake wee haya wee shauri yako.mtu hafanyi mchezo na kichaa kama yule