ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 28, 2014

JHIKOMAN, ZAWOSE, MAEMBE KUPAMBA ‘KARIBU FESTIVAL’

Px 1
Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
..Wapo pia Prof. Jay, Barnaba, Shilole
Na Andrew Chale
WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mapema Oktoba 27, Msemaji wa tamasha hilo Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema maandalizi yamekamilika na tayari wasanii wa awali waliopatikana wapo hadharani wanaendelea na matayarisho huku akiwaomba watanzania na wadau wa burudani kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.
Jazzphaa aliwataka baadhi ya wasanii wa nje na ndani na nchi zao katika mabano ni Panda (Japan), Maria Kate (Ufaransa), IFE Pianki (Uganda), Masayo (Japan), Fantuzz (Marekani), Shiwe Musique (Comoro), Dwembede (Kenya) na Mbiye Ebrima (Guinea).
px2
Mwanamuziki wa Msafiri Zawose anayepiga nyimbo za Cigogo, akionjesha vionjo vya moja ya nyimnbo zake kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho kwa wanahabari.
Makundi na majina ya wasanii kutoka nyumbani ni pamoja na Afrikabisa Band, Wahapahapa, Segere Original, Jahazi, The Spirit Band na Mama Africa.
Wengine ni Cocodo Band, Hokororo Band, Swanu Gogo Vibes, Swahili Vibes, Fimbo Band, Abeneko Music, Man Kifimbo, Saganda na Msafiri Zawose.
Wasanii wengine ni Msafiri Zawose ‘Chibite Zawose’, Tongwa Ensemble, Leo Manyika, Swahili Blues, Profesa Jay, Shilole, Juma Nature, Barnaba, Vitalis Maembe na Jhikoman.
Aidha, Jazzphaa aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo ni kukuza na kurasimisha tasnia ya muziki kwa umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo la Bagamoyo ambalo ni la kihistoria.
px 3
Mmoja wa viongozi wa kundi la muziki wa Pwani ‘taarab’ kutoka kundi la Jahazi, akiongea machache.
Kwa upande wa viingilio, alisema kitakuwa ni sh 5,000 kwa kila Mtanzania huku kwa atakayekata tiketi ya siku tatu, kwa pamoja, ni sh. 12,000.
“Tamasha hili litakuwa likifanyika usiku na mchana. Wasanii wote watakaokuwepo katika tamasha hili watalazimika kupiga muziki kwa kutumia ala za asili za muziki ‘Live’ na siyo ‘Playback’” alisisitiza Jazzphaa.
Kwa upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Richard Lupia alisema tamasha hilo mbali ya burudani, wasanii pia watapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuunadi muziki wao duniani kwa njia mbali mbali ambako kutakuwa na warsha kutoka kwa wataalamu toka pembe zote za dunia.

Pia alisema katika tamasha hilo kutakuwa na sanaa za Michoro, mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha.
“Semina na mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua nyingine za kimaendeleo zitatolewa kwa wasanii mbalimbali. Mbinu za kuuza kazi zao kwenye masoko ya kimataifa na kutafuta soko duniano kote hii itakuwa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa hapa hapa nchini” alisema Lupia.
px 4
Msanii nguli wa reggae, Jiko Manyika ‘Jhikoman’ akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
crew ya Karibu Festival na baadhi ya wasanii
Crew ya Karibu Festival na baadhi ya wasanii.

No comments: