Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza muda mfupi kabla wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hawajapigia kura ya kutaka vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha ambavyo Marekani imeiwekea Cuba viondolowe. nchi 188 zilipiga kura ya ndiyo, mbili zilipiga kura ya hapana na tatu zilipiga kura ya kutofungamana na upande wowote.
Na Mwandishi Maalum , New York
Kwa mwaka wa 23 sasa hapo
jana ( Jumanne ) Nchi wanachama
wa Umoja wa Mataifa wamepigia kura Azimio linaloitaka Marekani iondoe vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha dhidi ya Cuba.
Katika upigaji kura huo ,
nchi 188 ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilipiga kura ya ndiyo Azimio hilo
ambalo liliwasilishwa mbele ya wajumbe
na Waziri wa Mamb ya Nje wa Cuba, Bw. Bruno Rodriquez Parrilla
Marekani na Israel zenyewe
zilipiga kura ya hapana, huku
Micronesia, Marshall Islands na Palau
wakipiga kura ya kutoegemea upande wowote ( abstentions).
Akizungumza kabla ya upigaji kura huo kufanyika, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi
Ramadhan Mwinyi aliungana na wazungumzaji wengine katika kuitaka Marekani na Cuba
kumaliza tofauti zao za
kidiplomasia ili waweze kushirikiana na nchi nyingine katika kuzitafutia ufumbuzi
changamoto mbalimbali zinazomkabili mwanadamu.
Akasema dunia imeshuhudia namna
gani mataifa mengi yalivyojitoa muhanga
zikiwamo Cuba na Marekani ambapo wamepeleka wataalamu wao wa afya, wanajeshi
na vifaa ili kuukabili ugonjwa wa Ebola
katika nchi za Liberia,
Sierra Leone na Guinea ambazo zimeathirika vibaya kwa ugonjwa huu.
Akasisitiza kuwa mlipuko huo wa
Ebola umethihirisha namna gani mataifa yanavyoweza kushirikiana na kufanya kazi
kwa pamoja na kwamba mataifa
yanatakiwa kujenga mshikamano imara dhidi ya maadui wa binadamu na siyo kupingana
wenyewe kwa wenyewe.
Balozi Mwinyi akaongeza kuwa Tanzania
ambayo ni nchi rafiki kwa Marekani
na Cuba, kwa mara nyingine inasikitika
kusimama na kuzungumzia kuhusu
vikwazo hivyo ambavyo licha ya maazimio mengi kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa. Bado vikwazo vinaendelea.
Vile vile Balozi Mwinyi amesema hali ya kuendelea kwa vikwazo hivyo
kunasikitisha kutokana na sababu kuu mbili za msingi. Kwanza kuchelewa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo
kunadhoofisha hadhi ya Umoja wa Mataifa,
chombo chenye dhamana ya kuhifadhi Amani
na usalama wa kimataifa, kuhuisha
haki za binadamu, uchumi na ustawi wa wote.
Akasema inaposhindikana kutekelezwa kwa maazimio yanayopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni
kushindwa kwa wanachama wote.
Sababu ya pili ambayo amesema
inasikitisha ni kuona kuwa Nchi ambayo ilikuwa mwazilishi wa
Umoja wa Mataifa ( Marekani) inaendelea kupuuza wito ambao umekuwa ukitolewa
mara kwa mara, wito unaotolewa wanachama wa
Umoja wa Mataifa wa kutaka kusitishwa mara moja na bila masharti yoyote
vikwazo dhidi ya Cuba.
No comments:
Post a Comment