ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 25, 2014

GAPCO YAZINDUA KADI MAALUM ZA SAFARI ZITAKAZOWEZESHA DEREVA KUPATA UNAFUU WA BEI YA MAFUTA KATIKA VITUO VYOTE, TANZANIA

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari zitakazomuwezesha dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo vyote vya Gapco, Dar es Salaam jana.
 Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari zitakazomuwezesha dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo vyote vya Gapco, Dar es Salaam jana.
 Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akipongezana na Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto) baada ya kuzindua kadi maalum za Safari za kampuni hiyo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kutoka vituo vyote vya Gapco nchini kwa unafuu. Wengine (kustoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai, Ashok Dhar, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na Mkurugenzi wa kituo cha Gapco, Barabara ya Nyerere, Muntazir Bharwani.
  Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akikabidhi kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara na Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki baada ya kuzindua kadi hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika hafla iliyofanyika Kituo cha Mafuta Gapco cha Kamata, Dar es Salaam jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai, Ashok Dhar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok akionesha kadi maalum za Safari za Gapco baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kadi hizo zitamwezesha dereva kuweza kupata huduma ya mafuta kwa unafuu kutoka vityo vyote vya Gapco Tanzania. Kutoka kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Gapco Tanzania, Vijay Nair, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Diwani wa Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto), Meneja Miradi wa Gapco, Mohit Shirma, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
 Meneja Uendeshaji wa Kadi za Gapco, Shital More akielezea matumizi ya kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (katikati) baada ya kuzindua rasmi kadi hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika vituo vyote vya Gapco nchini katika hafla iliyofanyika kituo cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu, Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit Shirma, Rais wa kampuni ya Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar na maofisa wengine wa Gapco.
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa pili kulia) akifurahia jambo baada ya kuelekezwa matumizi ya kadi maalum za Safari Gapco na Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit Shirma baada ya kuzindua kadi hizo, katika kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
---
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM.
Kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa bidhaa za mafuta nchini, Leo imezindua programu aminifu kuwezesha wamiliki wa magari kujipatia pointi wakinunua mafuta ambazo zitawawezesha kupata ‘Mafuta Bure’ Kama faida.
Mpango huu utawanufaisha wakazi wa Dar es Salaam, kwa kuanzia na nchini kote mwakani.
Jerry Slaa, Maya wa Manispaa ya Ilala akizungumza katika sherehe ya uzinduzi iliyofanyika katika kituo cha GAPCO Kamata jijini Dar es Salaam alisema: "kuanzishwa kwa programu ya GAPCO Safari kutasaidia kutatua changamoto za muda mrefu zinazowakabili wamiliki wa magari nchini. Mfumo huu ni muhimu kuelekea jamii ya kufanya malipo bila fedha taslimu.”
Slaa alipongeza GAPCO kwa kuwa Kampuni ya kwanza katika sekta ya mafuta Kurudisha thamani ya fedha kwa wateja wake nakuomba Kampuni zingine kufuata nyayo za GAPCO.
Alibainisha kuwa huduma hii itasaidia kupunguza kwa ujumla, gharama za mafuta, kupunguza bugudha ya makaratasi na kusaidia kuendesha biashara kwa ufanisi zaidi.
Slaa aliongeza kwamba maendeleo kama hayo ni muhimu katika kuboresha uchumi wa nchi kwa kuwa usafiri ni moja ya nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania. Slaa alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuboresha sekta ya usafiri nchini.
Dr Macharia Irungu, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) GAPCO Group alisema GAPCO ina maslahi mapana katika soko la Afrika Mashariki na inajivunia kuwa na vituo vya mafuta 63 nchi nzima, na kuifanya GAPCO kuwa moja ya kampuni ya mafuta inayoongoza.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi kuzindua rasmi mpango, Bw. Ashok Dhar, Rais wa Reliance Industries Limited India, kampuni mama ya GAPCO Tanzania Ltd, alisema kuwa mpango huu unawakilisha sehemu ndogo ya faida ya GAPCO.
Bw. Dhar alisema anaimani na Uchumi wa Tanzania, na hivyo kampuni yake itaendelea kuwekeza zaidi nchini kwa miaka ijayo.
Akifafanua zaidi juu ya programu ya GAPCO Safari, Vijay Nair, Afisa Uendeshaji (COO) alisema kuwa kadi za Gapco Safari zitakuwa zinapatikana wakati wowote katika vituo vya mafuta vya GAPCO mkoani Dar Es Salaam kwa kuanzia.
mtendaji alieleza kuwa huduma hiyo ilikuwa wazi kwa wamiliki binafsi, kampuni na wafanya biashara ya magari.
"Tunataka kuboresha zaidi huduma zetu za uuzaji mafuta kwa wateja wetu. GAPCO tunaandhisha huduma ya kutoa huduma aminifu ambayo ni suluhisho kwa wamiliki wa magari nchini kote… Hii ni huduma ya kipekee tuliyo ianzisha tukiamini kupitia Kauli mbiu ‘……….’," alisema Bw Nair.

No comments: