Kaimu msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ), Meja Joseph Masanja, akizungumza makao makuu ya Jeshi, Ngome, Upanga jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba 13, 2014
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limekanusha vikali taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa kuwa, wanajeshi wake wanaoshiriki katika vikosi vya Umoja wa Mataifa chini Congo, vimewapiga raia wa Beni.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya JWTZ, Ngome, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Nov. 13, 2014, kaimu msemaji wa JWTZ, Meja Joseph Masanja, alisema uwepo wa JWTZ,huko Mashariki ya Congo, ni sehemu ya jeshi la Umoja wa Mataifa, (Force Intervention Brigade-FIB) lililopewa jukumu la kulinda amani Mashariki mwa nchi hiyo kubwa kabnisa na tajiri barani Afrika.
FIB linaundwa na majeshi kutoka Tanzania, Afrika Kusini na Malawi, na mwanzoni mwa wiki hii, palitopkea ghasia kwenye mji wa Beni, ulio mashariki mwa Congo, ambako watu kadhaa waliuawa na wavamizi wasiojulikana ingawa taarifa za kijasusi zinaeleza kuwa waasi wa kundi la Alliance for Defence Forces (ADF), kutoka Uganda, ndio bado wanaleta tabu kwenye eneo hilo na tyakriban miezi kadhaa sasa, vikosi vya jeshi la serikali ya Congo, (FARDC), vinavyosaidiwa na vile vya umoja wa mataifa, vinaendesha operesheni ya kukisafisha kikundi hicho.
Kaimu msemaji huyo wa jeshi aliwataka watanzania na dunia kwa ujumla kutambua kuwa, Tanzania iko Congo chini ya mwamvuli wa umoja wa Mataifa kufuatia azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa namba 2098 ya Machi 28 2013, ibara ya 9, linalotoa ruhusa kwa jeshi hilo kuhakikisha hali ya usalama na utulkivu ikiwa ni pamoja na kuwashinikiza waasi kusalimisha silaha zao vinachukua mmkondo wake.
“Kwa hiyo inakumbushwa na ieleweke kuwa, operesheni zote zinazofanyika huko, zinazingatia sharia na taratibu za umoja wa mataifa na si JWTZ kama jeshi pekee kama inavyovuma” alisisitiza Meja Masanja.
Wakati huo huo, JWTZ imesema kuwa yale mazoezi ya pamoja kati ya wanajeshi wa jshi la China na wenzao wa JWTZ, yatafungwa Ijumaa Nov 14, 2014 kule makao makuu ya kikosi cha wanamaji maarufu kama Navy Kigamboni.
Taarifa ya JWTZ ilisema, kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya kijeshi ikiwemo mazoezi ya baharini.
No comments:
Post a Comment