Kamanda Nsimeki aliwataja wakulima hao waliouawa ni Juma Omary (65) na Nyanya Ngoroka (70) wote wakazi wa Kijiji cha Cheka Nao, kata ya Kiperesa iliyopo mpakani na wilaya ya Chemba mkoani Dodoma. “Chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokea kati ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye shamba la wakulima hao na walipowakataza wakatumia silaha za moto na kuwakata mapanga wakafa papo hapo,” alisema Kamanda Nsimeki.
Alisema vifo hivyo vinatokana na kulipiza kisasi kati ya wafugaji na wakulima ambao chanzo chake ni migogoro ya ardhi ya muda mrefu. Naye, mkuu wa mkoa huo, Elaston Mbwilo alisema wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wazembe hawawajibiki katika nafasi zao na kuwa sehemu ya baadhi ya migogoro inayoendelea Kiteto. Aliyasema hayo mjini Kibaya akizungumza na wazee maarufu wa jamii ya wafugaji na wakulima, ili kujua kiini cha mauaji yaliyotokea Matui ambapo watu watano waliuawa kwa kukatwa mapanga. Mbwilo alisema wapo baadhi ya viongozi kuanzia ngazi ya Kata,Vijiji na Mitaa wamebeba uongozi bila kujua dhamana zao.
1 comment:
watanzania ufugaji wa kizamani umeshapitwa na wakati. wakati umefika serikali isisitize ufugaji wa kisasa. mtu amiliki ardhi aweke mifugo katika ardhi aliyomiliki. kuzurura na mifugo ndio kunasababisha mifugo kuharibu mashamba ya watu. sijui kwa nini serikali haiweki sheria kali kwa wale wanaolisha mifugo katika mashamba ya wananchi wengine au viongozi ndio wanabembeleza kura? shame on you!!
Post a Comment