Tafrani ilizuka katika mchana huu katika jengo la linalotumiwa na wafanyabiashara wadogo, maarufu kwa jina la Machinga Complex lililopo maeneo ya Ilala jijini Dar.
Mkuu wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi amethibitisha tukio hilo ambalo chanzi chake ni fundi aliyekuwa akichomea vyumba katika moja ya vizimba vilivyomo katika jengo hilo na kusababisha hitilafu ya umeme, uiliyoleta moto ambao umeunguza vizimba vitatu ndani ya jengo hilo.
Hata hivyo moto huo haukudumu kwa muda mrefu kwani kikosi cha Zimamoto, kwa kushirikiana na wafanyabiashara waliokuwa eneo la tukio wakafanikiwa kuuzima
...kuhusiana na hasara iliyotokea na jingine lolote kuhusiana na ajali endelea kufuatilia blog hii
Picha kwa hisani ya Mdimuz Blog.
No comments:
Post a Comment