ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 25, 2014

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MABALOZI NA WENYEVITI WA WILAYA MFENESINI CCM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM katika Wilaya ya Mfenesini.
Balozi wa Shina namba 36 Jimbola Mtoni Abdul-Aziz Salum akisoma risala ya Mabalozi wa Wilaya ya Mfenesini Kichama mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamuo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa Mgeni rasmi katika Mkutano Maalum kwa Viongozi hao akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja
Baadhi ya Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Wilaya ya Mfenesini Kichama wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi hao katika Ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi akiwa katika ziara zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi CCM Mikoa ya Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipofika katika viwanja vya Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Kihinani Mkoa wa Magharibi Kichama nje ya Mji wa Unguja kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Wilaya ya Mfenesini katika kuimarisha Chama katika wilaya hiyo. Picha na Ikulu.

No comments: