ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 14, 2014

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA:WANAFUNZI WATATU WA KIKE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WILAYA YA ILEJE.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya -SACP Ahmed Msangi
--
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WANAOSOMA SHULE YA MSINGI ILOMBA AMBAO NI 1. SEVELINA MWILE [11], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE 2. GRACE PATSON [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE NA 3. AGEY SEME [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ILOMBA[W] MBEYA VIJIJINI WOTE WANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULENI HAPO WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WAKATI WAKICHIMBA UDONGO NDANI YA SHIMO.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ILOMBA, KATA YA ITALE,TARAFA YA BUNDALI WILAYA YA ILEJE MPAKANI NA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI,MKOA WA MBEYA. 

AWALI KABLA YA KUKUTWA NA MAUTI WAHANGA HAO WALICHUKULIWA SHULENI NA ISAMBI MWASENGA [57], MWALIMU MKUU MSAIDIZI WA S/MSINGI ILOMBA KWENDA KUMFANYIA KAZI BINAFSI YA KUCHIMBA UDONGO NA KUMPELEKEA NYUMBANI KWAKE. MIILI YA MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA YUPO MAHABUSU KWA AJILI YA USALAMA WAKE WAKATI UPELELEZI WA SHAURI HILI UKIENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUWATUMIKISHA KAZI WATOTO WENYE UMRI MDOGO KATIKA MAENEO/MAZINGIRA HATARISHI YATAKAYOWEZA KUSABABISHA MAAFA NA KUFANYA VITENDO VYA NAMNA HIYO NI KWENDA KINYUME CHA SHERIA. 
 

Imesainiwa;
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: