ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 26, 2014

UPDATES YA MSIBA WA NDG SEBASTINA MGIMBA : MWILI WA MAREHEMU SEBASTIAN MGIMBA WAWASILI NCHINI JANA, MAZIKO KUFANYIKA LEO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

Msiba wa Marehemu Sebastian Mgimba upo Sinza Kumekucha ambapo baada ya mwili kupokelewa jana uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam umepelekwa Kwake Sinza na Hatimaye leoo Kutakuwa na Misa ya kumuombea marehemu na hatimaye Mwili wa Marehemu kupumzishwa Katika Nyumba yake ya Milele Katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe
 Ndugu pamoja na jamaa wa marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki dunia nchini Malaysia wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam eneo la Mizigo ukitokea nchini Malaysia.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki nchini Malaysia likiingizwa katika gari maalumu la kubebea jeneza katika uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam katika eneo la kutolea na kusafirishia mizigo mara baada ya mwili huo kuwasilini Nchini jana Novemba 25, 2014 ukitokea Nchini Malaysia.
Mchungaji akiendelea na ibada fupi iliyofanyika katika eneo la Kutolea mizigo katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam mara baada ya Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba kuwasili nchini leo.Picha zote na Josephat Lukaza - Wa http://www.josephatlukaza.com

No comments: