ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 14, 2014

Utawala kurejeshwa kwa Raia Burkina Faso

Muundo wa Serikali ya mpito nchini Burkina Faso umeridhiwa baada ya mazungumzo kati ya Viongozi wa siasa, Jeshi na Viongozi wa Asasi za kiraia.

Msemaji wa mazungumzo hayo mjini Ouagadougou amesema kuwa makubaliano hayo yamefikiwa kwa pamoja na Viongozi hao.

Uongozi wa mpito wa sasa umedhamiria kurudisha nchi kwa utawala wa kiraia na kujiandaa na uchaguzi mwakani.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Rais Blaise Compaore kushurutishwa kujiuzulu tarehe 31 baada ya maandamano makubwa.

Luteni kanali Isaac Zida alijitangaza kuwa Kiongozi wa Burkina Faso tarehe 1 mwezi Novemba baada ya Rais Compaore kutorokea nchini Ivory Coast baada ya kuwa madarakani kwa miaka 27.

No comments: