ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 29, 2015

BALOZI SEIF ALI IDDI AFUNGUA MKUTANO WA TISA WA TATHMINI YA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR

Makamu wa Pili w Rais wa Zanzibar Balozi Seifa Ali Iddi akifungua mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanizibar. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Muhammed Saleh Jidawi akizungumza katika mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta ya Afya kwa mwaka uliopita huko Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mwakilishi wa Shirika la WHO Zanzibar Dkt. Andymichael Ghirmany akizungumza kwa niaba ya washiriki wa maendeleo wa sekta ya Afya katika mkutano wa tathmini ya sekta hiyo Zanzibar katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufungua mkutano wa tisa wa tathmini ya Afya Zanzibar.
Washiriki wa maendeleo katika sekta ya Afya na baadhi ya waalikwa wa mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta hiyo wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo katika Hoteli ya Ocean Views Kilimani.
Naibu Katibu Mkuu wa Afya Zanzibar Bi. Halima Ali Maulid akitoa shukrani kwa niaba ya Wizara ya yake baada ya ufunguzi rasmi wa mkutao huo.
Dkt. Mkasha Haji Mkasha akitoa mada ya MKUZA namba mbili katika mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Ocean View.
Meza kuu katika mkutano ikiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakimsikiliza Dkt Mkasha alipokuwa akiwasilisha mada ya MKUZA namba mbili katika mkutano wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar pamoja na baadhi ya washiriki wa maendeleo na wageni waalikwa. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments: