ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 10, 2015

CHUCHU HANS AFUNGUKIA KUACHANA NA RAY

Staa wa Filamu Bongo, Chuchu Hans akiwa na mpenzi wake 'Ray''.


Stori: Musa Mateja na Gladness Mallya

STAA wa Filamu Bongo, Chuchu Hans juzikati alifungukia madai ya kwamba ameachana na mchumba wake Vicent Kigosi ‘Ray’, akaeleza kuwa, hakuna ukweli wowote juu ya hilo.Chuchu alifikia uamuzi wa kufafanua juu ya madai hayo juzi kufuatia tetesi zilizokuwa zimeenea kwamba yeye na kipenzi chake huyo wametibuana na sasa kila mtu kimpango wake.Akifungukia juu ya uvumi huo Chuchu alisema: “Kutakuwa na watu wanaosambaza uongo huo, huwezi kuamini muda si mrefu nilikuwa na baby wangu Ray, tukawa tunashangaa tu juu ya umbeya huo.
“Nahisi watu wamechukulia kwamba tumeachana baada ya mimi kuamua kubadilisha jina nililokuwa nikilitumia kwenye akaunti yangu ya kwanza ya Instagram, nimetoa neno The Greatest na kubakiza jina langu, ilikuwa ni uamuzi tu.
“Siwezi kuachana na Ray na hata kama ikitokea tumeachana naamini kabisa Ray hawezi kurudiana na Johari wala Mainda, hao wanaosema eti kaniacha mimi karudiana na Johari wanachemka,” alisema Chuchu.
CREDIT THECHOICE

1 comment:

Anonymous said...

well, kwanza kabisa huyo ray alishaa acha wanawake wangapi hadi kuja kwako? na kwa nini umesema hata kama mkia achana hawezi kurudi kwa johari? kwa huyo johari aliachwa ana nini na wewe usiachwe una nini haswa? sema ukweli sisi watu wa karibu tujuavyo kwa sasa kimenuka, jamaa kakuchoka huna mpango sio.so sepa bado na mapemaaaaaaa