ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 14, 2015

Kamati Kuu CCM chamaliza Kikao Chake cha Siku Moja Zenj

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakitoka katika ukumbi wa Mkutano baada ya kumaliza Kikao hicho cha kawaida cha Siku moja kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Wafanyakazi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kawaida cha Kamati Kuu kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai. Ali Vuai. baada ya kumalizika kwa Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM kisiwandui baada ya kumalizika kwa Kikao hicho cha siku moja kilichofanyika Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakitoka katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui baada ya kumalizika kwa Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu kilichofanyika Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Dk Jakaya Mrisho Kikwete. 
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi CCM,Ndg Nape akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM ilioyafa kikao cha Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. Zanzi News

1 comment:

Anonymous said...

Bwana Kimbisa, naona umeula!! I didn't know you were up there. Good luck!