ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 16, 2015

KINANA AENDELEA NA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA SPLM




Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya makundi hasimu. 

Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo 
Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto,Arusha. 
Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM.
Hapa wakiwa  na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti, na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kutoka kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali kutoka Sudani David Awet,Kiongozi wa wapinzani ndani ya chama cha SPLM Taban Deng na Deng Alor.

No comments: