ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 29, 2015

"Kuna Tatizo gani Lipumba Kupigwa Nawapongeza sana Polisi kwa Kumpiga"Hii ni kauli ya Lusinde Bungeni

Kulikuwa na mvutano mkali sana bungeni wakati wabunge wakijadili hoja ya Lipumba kupigwa. Hapo chini nimekuwekea michango ya Lusinde na Sadifa waliyoitoa Bungeni:
Lusinde: Kwani kupigwa Lipumba ndiyo tatizo, wamepigwa viongozi wangapi hapa, Lipumba siyo wa kwanza kupigwa
Lusinde: Nawapongeza Polisi safari hii kapigwa muhusika mwenyewe, ndiyo nzuri hiyo, siyo wapigwe wengine, kupigwa kazini ndiyo sawa

Lusinde: Bunge linapokwenda mwishoni wabunge wenye hali mbaya majimboni wanakuwa na hamsha hamsha ili wafikiriwe

Lusinde: Nawashauri wapiga debe mkiona watu wanaandamana magari hayatembei hampati pesa na nyinyi andamaneni.

Sadifa: Mnasema Lipumba kapigwa, hajapigwa hapo, kaguswa tu, huwezi kumlinganisha Lipumba na Kikwete.

8 comments:

Anonymous said...

Ukiona mwakilishi wa wananchi anatoa maneno kama aliyotoa Mh. Lusinde, basi ujue dhana ya woga, ubinafsi, kutojali na kukosa common sense vimetawala ndani ya serimali tawala na kwa vionvozi tunaowategemea.
Hii ni ishara mbaya Sana mfano potofu kwa kizazi kijicho.

Anonymous said...

Aibu tupu

Anonymous said...

Wewe uneangalia hapa Tanzania ukaona pana kiongozi? Tuna safari ndefu sana. Hawa polisi wanafurahia hongo kidogo tu na kufungulia majambazi toka kila upande. Sasa wenye macho wayafungue kuona kama hawa majambazi wanawaachia hiyo hongo. Watanzania tuache utani. Hii nchi inaangamia na viongozi wa CCM wanapigwa tu kuliko walivyotegemea. Kile walichomfanyia Lipumba na wengine kinajenga kizazi ambacho hakitamwachia hata mwenyiki wa kitongoji toka CCM aingie ofisini. Ipo siku nayo yaja "watapigwa tu" bilakujitambua. Mwenye macho haambiwi tazama haya Kikwete, Lusinde, Pinda na wengine mtajatuambia.

Anonymous said...

Ndugu hapo juu unayesema Tanzania haina kiongozi, sijaelewa msemo wako kabisa. Acha kuidhalilisha nchi yetu kwa fikra zako za bunuasi. Viongozi wetu wapo na wanafanya kazi kwa mwongozo wa katiba ingawa bado wana mapungufu makubwa. Kauli uliyoitoa haionyeshi kuwa una upeo wa mambo au mawazo yanayoendana na uhalisia. Kila serikali ina changamoto zake na suala la polisi kuvunja haki za raia hutokea katika kila nchi duniani na si Tanzania tu. Cha msingi iundwe tume huru ambayo itasaidia katika kuwawajibisha polisi wote waliotumia nguvu kuwaadhibu raia.

Anonymous said...

Kuunda tume ya nini? wakati kuna ushadidi wa kudhalilishwa kwa katiba ya nchi,ya Tanzania,maandamano sio kupigwa ,ulinzi wa raia na mali zao uko wapi<? unaye sema ni sawa hii sumu ya chuki ikienea kwa asilimia 100,hakuna atakaye ishi kwa amani,Mungu atusaidie,na mkuu wa mkoa,mwanasheria mkuu anaona ,ama kweli ,Mungu turehemu.

Anonymous said...

Kiongozi huwezi kusema hata siku moja acha apigwe,ni roho ya uuaji,na kutokujali,Mungu akusamehe tu Lusinde.

Anonymous said...

Hii ndio sababu viongozi na vyama vyote vya maruhani vitafanya kila njia kuhakikisha hakitoki madarakani kwani vinaelewa fika kwamba "What goes around comes around". Can you imagine if CUF or CHADEMA wakichukua madaraka what is going to happen? PAY BACK TIME

Anonymous said...

naungawa mkono na mdau mwenzangu aliyesame hii nchi haina kiongozi ni kweli haina kiongozi na aliye na upeo wa kuona mbali atalivumbua hili bila hata ya kuchukua darubini au mawani kuongaia kwa macho mawili ya ziada. na mimi naongezea NCHI IMESHAUZWAA KITAMBO TU NDO MAANA MAFISADI HAWATAKI KUWAJIBIKA NA WAKIWAJIBIKA WANATOA KASHFA ZAO.

Na si kweli chadema au cup ikuchukua nchi wata lipiza kisasa si watu wa visasi kama ma ccm walio wauwa wananchi walala hoi bila hatia huko arusha,dar,zanzibar etc

ukiwa ccm lazima uwe fisadi na ukikitetea lazima unajua kuna siku na wewe utakuja kupata mlo wa kifisadi hili halina mjadalaa.

na NDO MAANA KATIBA YAO WALIOICHAKACHUWA WANATAKA KUPITISHA ILI BAADAYE WANAOKWAPUA WASIKAMATWE WALA WASIWAJIBISHWE IWE TUMEKULA KWETU WANANCHI HAKUNA KUMKAMATA MKUU YEYOTE NA YEYE ANA ENJOY NA MAPESA YETU KWENYE MAHEKALU YAO.

NCHI HAINA KIONGOZI KILA MMOJA ANAJIFANYA YEYE NDO KIONGOZI ATAMUONGOZA NANI KILA MMOJA ANAHATIA YA UFISADI.

UKOO WA PANYA UNAZAA PANYA BUKU HUZAAI sisimizii(mdudu chungu).