ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 16, 2015

MAZIKO YA MUASISI WA CCM MZEE MAKAME SULEIMAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) akijumuika na Waislamu na Viongozi katika Kumswalia aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman katika Msikiti wa Ijumaa Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Marehemu alifariki jana Nyumbani kwake Amani Mjini Unguja. 
Wananchi na Waislamu wakilibeba Jeneeza la Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman aliyekuwa Mwenyekitiwa Wazee wa CCM na kuzikwa lao kijijini kwako Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katika) akijumuika na Waislamu na Viongozi katika Maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman aliyezikwa leo kijijini kwao Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman aliyezikwa leo kijijini kwao Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ikulu.

No comments: