Katibu Mwenezi na itikadi wa CCM DMV Bi. Salma Moshi ambaye pia alikuwa mshereheshaji wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM DMV Ndg. George Sebo akifungua mkutano Mkuu wa wanachama CCM DMV kwa kuwashukuru wanachama na kusisitiza kusahau yaliyopita na kutumia mwaka mpya wa 2015 kukijenga na kukiimarisha chama cha CCM DMV na kuwakumbusha wanachama kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na CCM DMV haina mgombea wa Urais inayemshabikia mpaka hapo atakapochaguliwa na Mkutano Mkuu wa NEC Tanzania nao wataunga mkono kwa nguvu moja.
Mratibu wa Vyama CCM Marekani Bi. Loveness Mamuya akisisitiza mshikamano wa Chama cha CCM Marekani na kuwaomba wana CCM DMV kutoa ushirikiano wa karibu kwa matawi mengine nchini Marekani kama vile wao wanavyokuwa karibu na Tawi la CCM DMV na kuwaomba wana CCM DMV kwenda New York kwenye shughuli yao ya miaka 38 ya kuzaliwa CCM itakayofanyika Februari 21, 2015 na pia alipendekeza shughuli kubwa za chama hicho nchini Marekani ziwe zinafanyika majimbo tofauti kwa lengo la kuwaweka wanachama wao karibu na kumwezesha mwanachama wa CCM popote pale awe karibu na chama chake.
katibu wa CCM DMV Bi. Jessica Mushala akielezea utendaji wa shughuli za CCM DMV za mwaka 2014 kuelekea mwaka 2015 Bi. Jessica Mushala alikuwa katibu wa tawi la CCM DMV siku ya uchaguzi mdogo Jumapili ya June 15, 2014 wa kujaza nafasi hiyo ilioachwa wazi na Bwn. Kinyemi ambaye kwa sasa anafanyakazi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na moja ya masharti ni usifungamane na upande wowote hasa inapokuja katika maswala ya siasa. Bi Mushala alimshinda mgombea mwenzake Ismail Mwilima kwa kura moja.
Katibu wa Jumuiya ya Vijana Bi. Grace akielezea Jumuiya yake na jinsi gani walivyojipanga mwaka huu kuwashawishi Vijana wa DMV kujiunga na chama.
Mwenyekiti wa Wazazi Auty Grace Mgaza Sebo nae akielezea majukumu ya Jumuiya yake na malengo ya jumuiya hiyo ya wazazi mwaka 2015.
Mama Kimolo Mwenyekiti wa UWT tawi la CCM DMV akielezea shughuli katika kitengo chake na jinsi gani watakavyojipanga mwaka huu wa 2015.
Katibu wa Shina la Maryland Germantown Ndg. Marco Mbullu nae alipata fulsa ya kuelezea Shina lake lililofunguliwa mwaka 2014 na Mwenyekiti wa Tawi CCM DMV ndg. George Sebo na kuzinduliwa na Mhe. Mwigulu Nchemba siku ya April 27, 2014.
Jabir Jongo akisisitiza mshikamano ndani ya chama CCM DMV na kuwaomba viongozi wakuu wa CCM DMV wajihusishe katika kuwaleta wawakilishi wa makampuni kama vile Bima maalumu kwa Diaspora WESTADI na kuielezea faida yake na kujaribu kuwashawishi wanachama wenzake kujiunga na bima hiyo.
Mama Kimolo nae aliwaeleza wanachama wa CCM DMV faida za PSPF huku akimgawia kadi ya uanachama wa PSPF katibu mwenezi na Itikadi tawi la CCM DMV bi. Salma Moshi.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Kutoka kushoto ni mratibu wa vyama Marekani Bi. Loveness Mamuya, Katibu wa shina la Maryland la Germantown Ndg. Marco Mbullu na Katibu wa tawi Bi. Jessica Mushala wakiwa katika mkutano mkuu wa wanachama CCM DMV uliofanyika siku ya Jumampili Januari 11, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn uliopo College Park, Maryland nchini Marekani.
Meza kuu kutoka kushoto ni Katibu wa shina la Maryland, Germantown Ndg. Marco Mbullu, Katibu wa tawi CCM DMV Bi. Jessica Mushala, Mwenyekiti wa Tawi CCM DMV Ndg. George Sebo, Mwenyekiti wa UWT Mama Kimolo na Mwenyekiti wa Wazazi Aunty Grace Mgaza Sebo.
2 comments:
ARE U KIDDING ME!!!
No, this is true!!! nyie wabongo wa USA mna muda na resources. How on earth utashabikia CCM, CUF au Chadema na wewe uko nje ya nchi?
Mtasimika mgombea next USA elections?
Post a Comment