Vijana 119 ambao walikamatwa katika msako wa Panya Road Wameachiwa na Polisi baada ya Kukosa Ushahidi wa Moja kwa Moja ambao unawahusisha na tukio hilo ..
Kamanda wa Polisi kanda ya Dar salaam Kova amesema japo wamewaachia wataendelea kufuatilia nyendo zao huko mtaani ,
Pamoja na Kuwaachia hao kamanda Kova Amesema Vijana 959 wamepandishwa mahakamani kwa tuhuma hizo za kujihushisha na kikundi cha panya Road
3 comments:
Tamasha la kiswahili .alianzisha Dj luke .watu wengine wanajifanya ndio wanalifungua .waswahili, bwana.
Kamanda mbona unalia imekuwajee??Panya kwelikweli!!
Ninaomba kutoa mawazo yangu kwa viongozi wa serikali kuhusu jinsi gani ya kusaidia vijana wetu ambao wamezagaa tu bila kazi za kuajiriwa au kujiajiri wenyewe. Kwanza kabisa si vijana wote wameweza kusoma kwa kiwango kikubwa yaani kufikia chuo kikuu.sasa basi serikali inatakiwa kupanga sera zote za kazi serikalini viwandani mashirika ya watu binafsi,kwamba kazi zipangiwe hata kwa vijana ambao hawana degree yaani zile kazi za chini zipangiwe kwa vijana ambao wana elimu ya chini yaani form your six wakipewa training watazifanya bila shida na hii itapunguza msongamano wa vijana wanaomangamanga mitaani. Vijana waliomaliza chuo kikuu wapewe kazi zajuu kidogo kufuatana na elimu yao.na siyo kumchukua kijana wenye degree na kumpatia kazi kwa mfano kazi ya data entry na kumlipa ajira kidogo,hapana hii kazi anaweza kuifanya hawa vijana wenye elimu ya chini na akaifanya vizuri .ni vema kushare kila mtu apate riziki yake ya kila siku.ninatumaini mtanielewa.
Post a Comment