ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 29, 2015

PROF. MBWETTE RAIS MPYA WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA PAN AFRICAN


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Tolly Mbwette amechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afrika (Pan African University) katika uchaguzi uliofanyika jijini Addis Ababa siku ya Jumatano tarehe 28 Januari 2015. Prof. Mbwette ambaye atahudumu nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo, aliwashinda wagombea wengine wanne katika kinyang’anyiro hicho.
Aidha, Bw. Ekwabi Mujungu amechagulikuwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Afrika inayoshughulika na mapambano dhidi ya rushwa kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
Uteuzi wao unatarajiwa kuthibitishwa na Walkuu Nchi na Serikali wa AU katika mkutano wao utakaofanyika Addis Ababa tarehe 30 na 31 Januari 2015. Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atashiriki mkutano huo.
Seikali kupitia Ubalozi wake wa Addis Ababa chini ya Balozi Naimi Azizi, ulipiga kampeni kuhakikisha kuwa wagombea hao wanashinda nafasi hizo

No comments: