Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akisoma hotuba fupi mbele za waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya Uzinduzi wa Mpango wa Kuuza Filamu za Proin Mtandaoni.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akisoma hotuba fupi kwa Mgeni rasmi ambae pia Ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh Dkt Fenella Mukangara wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kuuza filamu za Proin mtandaoni.
Muigizaji Emmanuel Muyamba Akiteta jambo na Mkurugenzi Wa Bodi ya Filamu Tanzania, ms Joyce Fissoo wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa filamu za kitanzania kupitia mtandao uliozinduliwa na kampuni ya Proin Promotions katika hoteli ya Southern Sun.
Na Josephat Lukaza
Mwishoni mwa Wiki Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Kazi za Filamu Tanzania ya Proin Promotions imezindua mpango wake wa kuuza filamu za Kitanzania kupitia Mtandao wahttp://www.proinpromotions.co.tz Filamu hizo za Kitanzania Kuanzia jana zimeanza kuuzwa katika mtandao wa Kampuni ya Proin Promotions (www.proinpromotions.co.tz) ambapo mpaka sasa tayari filamu zaidi ya kumi zipo mtandaoni.
Mbali na kuuza Filamu hizo Mtandaoni mteja pia anaweza kuangalia filamu hizo mtandaoni kwa masaa 48 huku akilipia gharama ndogo kabisa au akaamua kununua kabisa na kuimiliki filamu anayoitaka. Kampuni ya Proin Promotions imeamua kufanya hivyo ili kuweza kuwawezesha Watanzania wanaoishi ndani na nje ya Tanzania kuweza kupata filamu za Kitanzania kupitia mtandao.
Kampuni ya Proin Promotions imeamua kuuza filamu za kitanzania kupitia mtandao kwa lengo la kutanua wigo wa kuuza kazi zetu na kuwafikia wadau wengi zaidi duniani pamoja na kuzitangaza kazi zetu kimataifa.
Kampuni ya Proin Promotions inawakaribisha Wadau wote wa filamu nchini ambao wangependa kazi zao kuuzwa mtandaoni ili kuweza kuzitangaza na kuwezesha watanzania waishio ndani na nje ya nchi kupata filamu hizo kwa urahisi zaidi.
Proin Promotions imekuwa ni Kampuni ya kwanza nchini Tanzania ambayo imezindua huduma ya kuuza filamu za kitanzania kupitia mtandao huku wadau wengi wakitarajiwa kujiunga na Kampuni ya Proin Promotions kwa ajili ya Kuuza kazi zao kupitia mtandao.
No comments:
Post a Comment