ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 12, 2015

RIDHIWANI AZINDUA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MAGEREZA YA BWAWANI

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Bwawani katika Kijiji cha Visakazi Jimbo la Chalinze. Shule hiyo inamilikiwa na Jeshi la Magereza.
Ridhiwani akivishwa skafu na mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Bwawani alipowasili katika shule hiyo leo
Ridhiwani akiwa amekabidhiwa shada la maua
Ridhiwani akikgua gwaride la wanafunzi wa shule hiyo lililoandaliwa maalumu kwa ajili yake
Ridhiwani akilakiwa na maofisa wa Jeshi la Magereza
Ridhiwani akiwa na maofisa wa jeshi hilo Kaimu Mkuu wa Magereza, Emmanuel Lwinga na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Luganunulauu
Ridhiwani akihutubia wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Shule hiyo,Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Luganunula
Ridhiwani akiwa amekaa katika moja ya madawati yaliyomo katika moja ya vyumba vipya vya madarasa
Ridhiwani akikagua jengo hilo jipya
Ridhiwani akipanda mti wa kumbukumbu mbele ya jengo hilo

1 comment:

Anonymous said...

Are we serious, haya magwaride yana maana gani haswa?