Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ambae ameolewa na ana mtoto mmoja, amesema kuwa mara kadhaa anapokuwa kambini akishuti filamu mume wake, Dickson Matoke huwa anamfuata na kulala naye hadi asubuhi huku akiamini kufanya hivyo kunachangia kutochepuka.
Akizungumza na Uwazi, Shamsa alisema kuwa kitendo cha mumewe kumfuata haina maana kwamba wanavunja sheria zao bali hilo analifanya kwa kuwa yeye ni mke wa mtu na huwa anapewa chumba chake maalum.
“Mara nyingi ninapokuwa lokesheni kama si mbali na nyumbani basi naenda kumuona mume wangu na mtoto lakini kama ni mbali kidogo mume wangu huwa anakuja na kulala na mimi chumbani kwangu, asubuhi anaondoka naendelea na kazi yangu,” alisema Shamsa.
~Bongo Movies
1 comment:
mwache achunge ndoa yake lakin mtu akitaka kuchepuka atachepuka tu.mapenzi hayachungwi hata siku mmoja but kwa msimamo huu ninakupa kumii mwanangu shamsa ford shikilia uzi huu huu lala mwaya na mumeo halali yako na haki yake.
mungu aibariki sana ndoa yenu isingiliwe na shetani muovu.amen
Post a Comment