ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 9, 2015

SHUKURANI ZA DHATI

Familia ya Mwihava inapenda kutoa shukurani za dhati kwa kanisa katoliki la Mt. Edward Baltimore, Padri Honest Munishi,Padri Filbert Tairo, ndugu, jamaa na marafiki kwa kutumia muda wenu na kutufariji katika kipindi hiki cha msiba wa mpendwa baba yetu
Col. Clement Xavier Mwihava.

Shukurani zingine kwa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Col. Aldoph Mutta kwa kuwa na sisi bege kwa bega tangia siku ya kwanza ya msiba mpaka kanisani aliposoma wasifu wa mpendwa baba yetu ambao uliwagusa wengi.

Shukurani kwa kamati ya maadalizi kwa kazi nzuri iliyofanya ya chakula na vinywaji hususani kanisani.

Pia tunapenda kuwashuku wote waliopiga simu baada ya kupata taarifa hizi za msiba na shukurani pia kwa ambao walishindwa kufika kutokana na majukumu mengine tunaelewa nia na mioyo yao ilikuwa pamoja nasi katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu Ahsanteni sana. Baba amepumzika sasa mahali pema. Cane, Derick na Neema tunasema "Ahsanteni sana" 

Hatuna tutakachoweza kuwalipa kitakacholingana na yote makubwa mliotufanyia na kusema ahsante haitoshelezi na wala haina uzito utakao lingana na yale yote mlioufanya juu yetu na sisi kujisikia tumefarijika sana. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awazidishie mara dufu  Ahsanteni na Mbarikiwe sana.

No comments: