Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akiandika salamu za rambirambi kufuatia tukio linaloelezwa kuwa la kigaidi ambapo watu kumi na mbili wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo waliuawa.
Balozi Tuvako Manongi akibadilishana mawazo na Mabalozi wenzie muda mfupi kabla ya kusaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio la jumatano ambapo watu kumi na mbili wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo walipoteza maisha
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, jana Ijumaa alijumuika na Wawakilishi wa Kudumu wa Mataifa mengine katika Umoja wa Mataifa, waliojitokeza katika kile kinachoweza kuelezwa kama mshikamo kusaini kitabu cha Maombelezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Ufarasa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio linaloelezwa kuwa la kigaidi lililotokea siku ya Jumatano ambapo watu kumi na mbali wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo walipoteza maisha katika shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment