ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 13, 2015

Waandishi wa habari nchini Uganda waandamana kudai mazingira salama ya kufanya kazi.

Mwandishi wa habari aliyepigwa na kujeruhuwa akiwa kazini amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Msambia, nchini humo.
 Waandishi wa habari nchini Uganda waandamana kudai mazingira salama ya kufanya kazi.
 
Moja ya story zilizochukua headlines kutoka Uganda leo January 13, ni ile inayohusu Waandishi wa habari nchini humo kuandamana baada ya Afisa wa Polisi Joram Mwesije, kumpiga mwandishi Adrew Lwanga, na baadae akakutana na Ispekta wa Polisi na kukiri makosa yake, pamoja na kukubali kulipia gharama zote za matibabu za mwandishi huyo.

Waandishi hao waliandamana hadi makao makuu ya Polisi na kutaka kukutana na mkuu wa Polisi kwa lengo la kuhakikishiwa mazingira salama ya kufanya kazi, baada ya mwandishi mwezao kupigwa na kujeruhiwa vibaya na Afisa wa Polisi, Maandamano yaliyoanza baada ya kikao walichoafikiana kutokuandika habari zozote kuhusu shughuli za Polisi hadi Afisa aliyefanya tukio hilo akamatwe na kuachishwa kazi.

“Likuwa mbaya sana hiyo Journalist hiyo ni watu wa kusave hii nchi yetu sasa kuona hiyo mambo ya kupiga Journalist tuliona hiyo kitu ni mbaya, sasa tulisema tunataka tutembee tufike huko Naguru tuone IGP, tumuambie kila kitu tumeona hapa Journalist tunataka kupigwa sasa watuache tufanye kazi yetu.
“-CREDIT:MILLARD AYO.COM

No comments: