ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 15, 2015

WANNE WAFA WAKIHOFIA KUTOKEA AJALI HUKO PWANI

WATU wanne wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Abiria la Hajees likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam na lori katika eneo la Mandera Mkoani Pwani leo asubuhi.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrich Matei amesema kuwa abiria hao waliruka kutoka katika basi hilo kuhofia ajali ya kugongana na lori lililokuwa likitokea mbele ya basi hilo na ndipo walipoangukia barabarani na kupelekea vifo vyao, baada ya dereva wa basi kutoka nje ya barabara.

Aidha Kamanda Matei amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wa Chanzo cha ajali hiyo wanamshikilia dereva wa lori hilo ambalo lilisababisha vifo vya abiria hao walioruka kutoka katika basi la Hajees.
GPL

No comments: