Bobbi Kristina akiwa na Nick Gordon
Bobbi Kristina alikutwa siku ya Jumamosi akiwa amenguka bafuni akiwa ameinamisha kichwa chini huku akishindwa kupumua na kudhaniwa kudhulika na madawa ya kulevya. Madaktari wameeleza kwa sasa hali yake inatia matumaini na oksigeni imeaanza kuongezeka kwenye ubongo wake kitu ambacho apo mwanzo hakikuwepo.
Madaktari wanaoendelea kumtibu wamesema siku alipofikishwa hospitalini hapo ubongo wake ulikua unafanyakazi kwa kiwango cha chini mno kutokana na kuishiwa hewa aina ya oksigeni kitu ambacho ni hatari kwa mwanadamu na kama wasingemwahisha hospitali sasa hizi ingekua ni habari nyingine tuzidi kumwombea apone haraka.
Familia ya Bobbi Kristina imeeleza kwamba Polisi waliporudi kwa mara ya pili kupekua nyumba ya Bobbi Kristina walikuta madawa kwenye chumba cha mtoto huyo wa Witney Houston kitu ambacho Polisi wenyewe hayajasibitisha japo walishuku tangia mwanzo kwa hali waliyomkuta nayo Bobbi Kristina iliwezekena ilisababishwa na kubwiya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment