ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 19, 2015

JESSICA MUSHALA, LOVENESS MAMUYA NA CHRIS LUKOSI WAKANUSHA HABARI KUHUSIANA KUTANGAZA VITA BAADA YA KUKOSA UKUU WA WILAYA

Bi. Jessica Mushala          Bi. Loveness Mamuya              Bwn. Chris Lukosi

Habari iliyoandikwa leo kwenye mtandao wa Jamii Forums na mdau ambaye hakujitambulisha jina na baadae kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ikiwemo SMS na Whatsup iliyobeba kichwa cha habari "Makada wa CCM Diaspora watangaza vita baada ya kukosa ukuu wa Wilaya"

Vijimambo ilibidi iwavutie waya kwa nyakati tofauti wahusika wakuu waliotajwa kwenye habari hoyo kutaka kujua kulikoni na kama habari yenyewe ina ukweli ndani yake. Kwanza ilianza kwa kumtafuta Katibu wa CCM DMV Bi. Jessica Mushala ambaye Januari 25, 2015 aliwasili Tanzania kwa ajili ya kutoa semina kwa wafanyabiashara wa Tanzania ambao wangependelea kuingia ubia na wafanyabiashara au makampuni ya Kimarekani na hizi ndivyo alivyosema
Vijimambo haikuishia hapo iliendelea kumtafuta mratibu wa matawi ya CCM Marekani Bi. Loveness Mamuya naye alianza kwa kusema kwamba habari hizo ni za kizushi na udaku wa hali ya juu na kila kitachoandikwa Jamii Forums ukianza kukikanusha, utakanusha vingapi habari hiyo imesema tutasusia sherehe ya CCM New York basi tusubili tuone kama tutaenda au la. Mtandao wa Jamii forums wakati mwingine unakua na habari zisizo sahihi na za kidaku. Mimi sioni sababu yakupoteza muda na sauti yangu eti ninakanusha habari iliyoandikwa Jamii forums na nashukuru kwa kuchukua muda wako kunipigia na kutaka kujua ukweli wa habari hi.

Vijimambo iliendelea na jitihada za kumtafuta Chris Lukosi ilimpigia simu yake ya mkononi ya UK na kukuta imezimwa na baadae ikamtumia ujumbe mfupi na yeye akajibu kwamba kwa sasa yupo Dar es Salaam, Tanzania na akatoa namba yake ya kiganjani ya Dar na Vijimambo ikamvutia waya kutaka kujua upande wake anasemaji kuhusiana na habari hiyo iliyotikisa mitandao ya simu za mikononi huku watu wengine wakiamini kwamba habari hiyo ina ukweli ndani yake.

Chris Lukosi naye alikanusha habari hiyo na kusema yeye aliambiwa na marafiki zake na baadae alipoingia jamii forums alikuta imeisha tolewa huku akiongea kwa masikitiko kuhusiana na habari hiyo kwa kusema mtu anaweza kuamka na kukosa kazi na kuamua kujitungia habari ya uongo namna hiyo kweli kuna wabongo wengine hawana kazi za kufanya.

Chris Lukosi aliendelea kwa kuishukuru Vijimambo kwa kutafuta ukweli wa jambo hilo na kusisitiza huku akimalizia kwa kusema habari hizo ni uzushi mtupu na ninalaani vikali mwandishi wa habari hiyo badala ya kujenga jamii anaandika habari ya kupotoshaji hasa katika muda huu wa kuelekea kipindi cha uchaguzi.

No comments: