HUDUMA ya maji safi na salama katika kisiwa cha Kojani wilaya ya wete Pemba, imekuwa ni ya saa 24, jambo ambalo wananchi wake wamekuwa wakilifurahia, ingawa utumiaji mbaya wa miundombinu hiyo kwa kufungua bomba (mfereji) hadi mwisho kwa mahitaji kidogo ya maji imekuwa changamoto kwa baadhi ya wananchi.
MTOA mada ya usafi wa mazingira (katikati mwenye miwani) Bakar Hamad Bakari akiwaeleza wananchi wa kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete Pemba, jinsi ya umuhimu wa kutenganisha taka ngumu na laini, baada ya wananchi hao kupewa mafunzo ya usafi wa mazingira kupitia jumuia ya vijana Jimbo la Kojani KOYMOCC.
KUTOKANA na upepo mkali unaoendelea kuvuma, wananchi wa Kisiwa cha Kojani wilaya ya wete Pemba, na wao wamechukuwa na tahadhari kwenye vyombo vyao vya usafiri, kwa kupunguza idadi ya abiria ili kujikinga na upepo mkali, ambapo dau kama hili kwa siku za kawaida hubeba takriban abiria 30.
MOJA ya sababu zilizotajwa na baadhi ya wazazi wa Kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete Pemba, kwamba huwakimbiza watoto wao skuli ni uvuvi na michezo kama ya keram, ambapo watoto hawa walinaswa na kamera ya Zanzibar leo wakicheza mchezo huo, wakati ambao wenzao wakiendelea na masomo skulini na madrassa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment