Mwili wa marehemu Salmin Awadhi ukipakiwa gari tayari kwa taratibu za mazishi hapo leo, katika makaburi ya makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, mwili wa marehemu unategemewa kuagwa kesho saa tano katika ukumbi wa baraza la wawakilishi Chukwani Unguja na kusaliwa katika Masjid Muhammad kwa mchina na kuzikwa Kijiji kwao Makunduchi Unguja
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika nyumbani kwao marehemu mtaa wa mpendae kupata habari ya msiba huo. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg Vuai Ali amesema marehemu alifika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa kazi zake na kuhidhuria Kikao cha Sekreteli kilichofanyika asibuhi hofisini hapo , na kusema marehemu ametoka chumba cha mkutano na kwenda Afisi kwake ya Mnadhimu wa CCM Baraza la Wawakilishi, ndipo matatizo yalipojitokeza na kusema anasikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa matibabu , kufika huko hali ilibandilika na kufariki dunia. Marehemu ameacha pigo kwa Chama na wananchi wa jimbo lake.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mussa , akiwa katika eneo la msiba akizungumza na ndugu na jamaa wa marehemu katika kupanga taratibu za msiba.
No comments:
Post a Comment