Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
STORI: Mwandishi Wetu/Amani
IMEKULA kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.
Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.
WASIKIE WENYEWE
“Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.
“Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake.”
Akaongeza tena: “Kama sijasahau hata kwenye kifo cha mwanamuziki wa Bendi ya Msondo, marehemu Maalim Gurumo hakutokea japokuwa alikuwa amerudi nchini kutoka nje. Magazeti mliandika kwamba Wema alimzuia kwenda kuzika. Sasa ni vizuri kweli?”
WANAOTOA POLE KWENYE MITANDAO
Wakati wasanii hao wakimchana Diamond, wasanii wa filamu, Tamrina Poshi ‘Amanda’, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha wao walisema wanakerwa na tabia ya baadhi ya wasanii kutohudhuria misiba ya wenzao na kuishia kutoa pole kwenye mitandao ya kijamii.
Wakizungumza na Amani, wasanii hao walisema imekuwa ni kawaida kwa wasanii kutohudhuria misibani bila kuwa na sababu na kuongeza kuwa tabia hiyo si nzuri kwa umoja wao.
AMANDA
AMANDA
“Mfano mzuri tunauona hapa leo, mwenzetu kafiwa na baba yake ukiangalia wasanii waliohudhuria wanahesabika lakini nimepata mshangao kwa sababu rafiki mkubwa wa Dully ni Diamond lakini hapa hajaonekana. Tunaona tu pole zinaishia kwenye mitandao. Mtu yupo Zanzibar tu hapo na anatupia picha akiwa na mpenzi.”
BELA NAYE
Kwa upande wake, Bela alisema alipata taarifa za msiba huo akiwa hospitali amelazwa lakini akaona ni vema ahudhurie mazishi kwa kuomba ruhusa kwa daktari pamoja na kuwa hali yake haikuwa nzuri.
“Nilikuwa nimelazwa na niliwekewa dripu kabisa baada ya kugundulika nina malaria tano, lakini nikaona siwezi kukosa kuhudhuria msiba kwa sababu marehemu mzee Sykes mbali ya kuwa baba yetu alikuwa mshikaji wetu sisi wasanii,” alisema Bela.
BABY MADAHA.
BABY MADAHA
“Jamani hili jambo lisikieni tu kwa watu, mimi sikuamini kwa sababu siku siyo nyingi Dully aliniambia baba yake anaumwa miguu na walikuwa kwenye mipango ya kumpeleka India akatibiwe, kumbe baadaye hali ilibadilika mpaka umauti ukamkuta, nimeumia sana.
“Wasanii tuache ‘u-snich’ (unafiki) kwa sababu wengi wetu wanaishia kuandika kwenye mitandao tu mi sidhani kama hiyo ni faraja, faraja ni kumfariji mwenzetu tena kwa ukaribu.”Diamond alipotafutwa kwa njia ya simu alisema: “Hata mimi nimeumia kwa kifo cha baba’ke Dully lakini si kwamba sijakwenda makusudi, nilikuwa na dharura.”
Mzee Sykes (pichani) alifariki dunia, Jumapili ya Februari 15 katika Hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa akisumbuliwa na presha. Alizikwa Februari 16 katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake