Mhe. Mjenga alimkaribisha Mzee Sambi, Rais Mstaafu wa Comoros
Mhe. Omar Mjenga, amewaandalia chakula cha jioni Waheshimiwa Janet Mbene, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar ambao wamekuwepo Dubai kwa ziara ya kikazi.
Aidha, katika hafla hiyo, Mhe. Mjenga alimkaribisha Mzee Sambi, Rais Mstaafu wa Comoros. Wageni wengine waalikwa ni pamoja na Ndugu Joseph Kusaga na familia yake, Mfanyabiashara Hashimu Lema kutoka Tanzania, Bwa. Islam Balhabou na Bw. Cleophas Ruhumbika, Mkuu wa Kituo cha Biashara, kilichopo katika Ubalozi Mdogo.
Mhe. Omar Mjenga akiwa na wageni wake alipokuwa amewaandalia chakula cha jioni.
Balozi mdogo Dubai Mhe. Omar Mjenga katika picha ya pamoja na wageni wake.
wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja.
wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja.
I don't know this guy but he is doing a great job in Dubai, keep up the good work!
ReplyDelete