Mwanadada mrembo akipozi kwenye eneo maalum kukaribisha mashabiki wa Skylight Band kwa shots za Zappa na Tequila pamoja na ua aina ya Rose maalum kuonyesha upendo kwa wapenzi wao katika usiku maalum wa wapendanao uliofanyika jumamosi iliyopita ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village....Skylight Band itaendelea kusambaza upendo Ijumaa ya leo, baada kurejea nyumbani salama wakitokea nchini Oman....Muda ule ule... uchakavu ule ule... mahali ni pale pale....Karibuni.
Mkali wa R & B Skylight Band, John Music akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo kwenye usiku maalum wa wapendanao (Valentine's Night Party) iliyofanyika siku ya Jumamosi ikiwa lengo la kusambaza upendo kwa mashabiki wao Valentine's day. Kulia ni Ashura Kitenge na kushoto ni Baby wakipiga back vocal kumsapoti John Music.
Ashura Kitenge akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band sambamba na kusindikizwa na Baby.
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akitoa burudani kwa hisia kali ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar kwenye usiku maalum wa wapendanao ulioandaliwa na bendi hiyo. Katikati ni Aneth Kushaba AK47 pamoja na Sam Mapenzi wakimsindikiza Sony Masamba.
Mashabiki wa Skylight Band wakisakata rhumba siku ya maalum ya usiku wa wapendano nao iliyofanyika ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe wa muziki wa Live Joniko Flower akiwachezesha ligwaride waimbaji wenzake kwenye usiku maalum wa wapendanao uliofanyika ndani ya kiota cha Thai Village, mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Sam Mapenzi, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Sony Masamba.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiitikia ligwaride la rapa Joniko Flower na style za aina yake.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo kwenye usiku maalum wa siku ya wapendanao sambamba waimbaji wenzake, Kutoka kushoto ni John Music, Baby pamoja na Ashura Kitenge.
Waimbaji wa Skylight Band na sura zilizojaa furaha na upendo ndani yake kwa mashabiki wao.
Mashabiki wakionekana kukunwa na burudani ya Skylight Band.
Skylight Band wakiendelea kulisongesha...ni Ijumaa hii tena na sio ya kukosa....See you later...!
Ilikuwa full mzuka...kama inavyoonekana pichani....When Jesus say Yes.....No Body Can Say No...... si mwingine ni Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani adimu kwa mashabiki wa Skylight Band.
Mpishi bora wa muziki wa Skylight Band anafahamika kama Idrissa Drums akitweta jasho wakati akiwajibika jukwaani.
Mashabiki wakiendelea kuchiziki na burudani ya Skylight Band.
Sam Mapenzi akiwaongoza mashabiki wa Skylight Band kwenye burudani ya aina yake katika usiku maalum wa siku ya wapendanao ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar...Usikose Ijumaa hii mwendo ni ule uleeeee.
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwa raha zao.
Digna Mbepera akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band katika usiku maalum wa siku ya wapendanao ndani ya kiota cha Thai Village-Masaki jijini Dar huku Ashura Kitenge na Sony Masamba wakipiga back vocal.
Pichani juu na chini ni mashabiki wakisebeneka na burudani ya aina yake kutoka Skylight Band.
Visura wa Skylight Band wakipata Ukodak.
Kutoka kushoto ni Ema Bass, Tophy Bass pamoja na Danny Kinanda wakishow love na ukodak.
Binti mrembo mwenye kipaji cha aina yake Digna Mbepera akishow love na Ukodak.
Kisura mwingine wa Skylight Band anafahamika kwa jina la Baby katika pozi matata sana.
Sam Mapenzi akipata ukodak na mdau King Kif aliyeambatana na mdogo wake.
Mdau wa Skylight Band akipata ukodak ndani ya kiota cha Thai Village-Masaki jijini Dar....Ni Ijumaa hii tena tukutane pale na maukodak yakumwaga.
Mdau Mulle wa Skylight Band akishow love na swahiba wake ndani ya kiota cha Thai Village-Masaki jijini Dar.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake