Na Mwandishi
Maalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon amemteua Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe.
Mohamed Chande Othman kuongoza jopo huru la wataalam watakaopitia taarifa
mpya kuhusu kifo cha Bw. Dag
Hammarskjold ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
“ Katibu Mkuu
anayofuraha ya kutangaza kwamba amewateua
wafuatao kuwa wajumbe wa jopo huru la
wataalamu. Bw. Mohamed Chande Othman
kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atakuwa mkuu wa jopo hilo. Wajumbe
wengine ni Bw. Kerryn Macaulay kutoka
Australia na Bw. Henrik Ejrup Larsen kutoka Denmark” inasomeka taarifa iliyotolewa
na Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu
Uteuzi wa Jopo hilo
unatokana na Azimio namba 69/246 la
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
lililopitishwa tarehe 29 mwezi Desemba 2014
ambalo lilimtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuteua jopo la
wataalam huru ili kuchunguza na kutathimin thamani ya taarifa mpya ( probative
value)zinazohusiana na kifo cha Katibu
Mkuu Dag Hammarskjold pamoja na watu waliofuatana naye.
Bw. Dag Hammarskjold na
ujumbe wake alipoteza maisha katika ajali ya
ndege iliyotokea mwaka 1961 wakati akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baadhi ya Majukumu ya Jopo hilo huru la wataalamu
pamoja na mambo mengine yatakuwa kupitia
na kutathmini thamani ya taarifa mpya
ambazo Kamisheni ya Hammarskjold imeziwasilisha
kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Vile
vile litatathmini taarifa mbalimbali ambazo zimetolewa na nchi wanachama na vyanzo vingine.
Jopo hilo la wataalam
huru litaanza kazi yake mwisho mwa mwezi huu wa March ( 30 March) na linatarajiwa
kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu
Mkuu si Zaidi ya tarehe 30 mwezi
June mwaka huu.
No comments:
Post a Comment