ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 18, 2015

CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA KUTILIANA SAINI NA INDIA

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiwaelezea Waandishi wa Habari jinsi alivyofurahishwa na maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akimsalimia mwanafunzi wa Udhamili katika Takwimu Rasmi Happiness Katuma wakati akikagua baadhi ya vitu mbalimbali kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akipitishwa katika maeneo mbalimbali ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha Takwimu cha nchini India
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akimwelezea Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal kuhusu chumba cha kompyuta kilichopo chuoni hapo wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO

No comments: