ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 15, 2015

Florah mbasha: Nipo Tayari Kurudiana na Mume Wangu.

Muimbaji wa muziki wa injili, florah mbasha amesema yupo tayari kurudiana na mume wake emmanuel mbasha, ikiwa atakwenda kumuangukia mguuni na kumuomba msamaha.
Florah alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa ushahidi mahakamani juu ya kesi ya ubakaji inayomkabili mume wake ambayo inasikilizwa katika mahakama ya wilaya ya ilala.

"Mbasha nimeshamsamehe siku nyingi na nipo tayari kuishi naye iwapo atakuja kuniangukia miguuni na kuniomba msamaha..lakini hili la ubakaji ni suala la mahakama" Alisema.

4 comments:

Anonymous said...

Hiyo sio kusamehe kama unavyodai eti akuangukie miguuni kwani ww Mungu??yaani watu wengine mnapenda kuabudiwa kweliii halafu unajiita mkristo,wa kuangukiwa miguuni ni Mungu pekee dada.

Anonymous said...

huyu atakuwa mwanaume aliyeachana na mke wake.

Anonymous said...

ujamsamehe bali kuna unachikihitaji zaidi. eti ulishamsamehe halafu unathubutu kusema akuombe msamaha na kukuangukia miguuni!!!!!!!! dah! wala hata hatukuelewi, hata wasiomjua Mungu hawajikwezi hivyo sembuse wewe unaejiita umeokoka.

Anonymous said...

Mwanamke mwenye busara ndo hujishusha na kumwangukia mumewe. Jiangalie mwenyewe kwanza ni makosa mangapi umeyafanya na bado mumeo alikwa na wewe. Fuata maadili ya kitanzania km kweli wewe ni mke mwema tena unajiita mkristo km siyo usanii wa kujivika ukristo wakati ndani yako hauko msafi.