Matokeo ya awali yalionyesha chama cha mrengo wa kushoto cha Zionist Union kupata mshitiko.
Huku kura nyingi zikiwa zimehesabiwa, Likud kinaonekana kupata viti 29 katika bunge lenye viti 120, huku chama cha Zionist Union kikiwa na viti 24.
Matokeo haya yakithibitishwa, itaonyesha kuwepo kwa serikali nyingine ya mseto itakayoongozwa na Bwana Netanyahu.
Bwana Netanyahu atahitaji kuungwa mkono kutoka vyama vingine ili kuunda serikali ya mseto.
Katika hotuba kwa wafuasi wake mjini Tel Aviv baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura Jumanne, Bwana Netanyahu amesema tayari amezungumza na viongozi wa vyama vingine vyenye mrengo wa kulia kuhusu kuunda serikali mpya "bila kuchelewa".
Bwana Netanyahu amehodhi siasa za Israel kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka 20.
Kiongozi wa muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto wa Zionist Union Yitzhak Herzog amekishutumu chama tawala cha Likud kwa kudidimiza viwango vya maisha ya raia wa Israel na amekuwa akipiga kampeni dhidi ya sera za nje za Bwana Netanyahu.-BBC
No comments:
Post a Comment