Rais Dilma Roussef wa Brazil
Zaidi ya watu milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe mashtaka ya ufisadi mkubwa uliofanyika katika shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia.
Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani.
Mmoja wa waandamanaji Francisco Pestana alilalama akisema"Dilma hana uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tunachokabiliwa nacho ni bahati mbaya sana, namna mamabo yanavyokwenda, yanaweza kuelekea kubaya zaidi, tutakuwa Venezuela nyingine."
Naye mwandamanaji mwingine mwanamke Janaina Lima anasema "leo ni maandamano ya watu. Watu wamejitokeza mtaani kusema hakuna ghasia zaidi, hakuna rushwa, hakuna uvivu zaidi, hakuna uzembe zaidi, hakuna utawala mbaya. Na kuunga mkono Brazil mpya."
2 comments:
Watanzania tufuate mfano wa Brazil. Wala rushwa, wala escrow, wavivu, na utawalawa mbaya hawana nafasi Tanzania. Maandamano ya watu bila ghazia yanaweza kuondoa ufisadi na kuimarisha uongozi bora Tanzania na Africa
bendera ya brazil inafanana na bendera ya Tanzania. Kwa hivo tuna matatizo yanayo fanana. Brazil wana mafuta mengi sana na tanzania tuna gas nyingi sana. Kitu kinachkwaniza hizi nchi kuendelea ni usifadi mkubwa.
Tanzabrazi against corruption movement.
Post a Comment