ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 16, 2015

YA MOTO BAADA YA KUWAPAGAWISHA UK SASA NI ZAMU YA NEW YORK FRIDAY MAY 22. NA 23 DC









YA MOTO BAND LIVE NEW YORK NA WASHINGTON DC. KWA UDHAMINI WA TEMBAPHOTO & 0VIJIMAMBO. KWA TAARIFA ZAIDI YA UJIO HUU WA YA MOTO BAND ENDELEA KUFATILIA KUPITIA VIJIMAMBO NA WWW.TEMBAPHOTO.COM
HUU NI UKUMBI WATAKAOWASHA MOTO VIJANA WA YA MOTO BAND NEW YORK CITY FRIDAY MAY 22 NA WASHINGTON DC MAY 23.

Kwa wale wa V.I.P hii ndiyo sehemu yao wakiwa na Bottle of Champagne.
Ukumbi upo Harlem Opsite  ya Apollo Theater New York City na pia Opsite ya State Office Building.

27 comments:

Anonymous said...

Sisi tunataka kucheza rhumba kwahiyo tupelekeni sehemu ambayo tutacheza bila bughudha.mwisho saa kumi alfajiri (4am).sio sehemu ikifika saa sita usiku mnaanza kutafutana.

Anonymous said...

Tarehe jamani. Wengine mpaka turequest a month in advance.

Anonymous said...

inchi yenu inaangamia nyinyi mko majuu mnachezeshwa ya moto haaaaaaaaaaa
kweli mijutu nyinyi wa marekani sijui nikuiteni vipi.si mlitoka huku huku nyumbani na kulaani maisha ya huku sasa mko majuu badala kufanya mambo yahuku kwenu kila leo mnayatafuta ya nyumbani.

bora si mrudi.le mutuz William malecela huwa anasemaga ukweli mnatukana na kumsema bure.

maisha magumu rudini kwenu mcheze ngoma vya vigodoro na yamoto na ya baridi pia tunayoo kazi kwenu.

Anonymous said...

hiyo nchi yenu inaangamia kwa uzembe wenu wenyewe. huyo aliyelaani maisha ya bongo labda ni yule ndugu yako aliyekataa kukutumia barua ya mwaliko na wewe ung'aze macho kidogo. majuu kila mtu alikuja kwa ustaarabu wake mwenyewe, usitulinganishe na lemutuz aliyeingia majuu kwa kuzamia meli na alivyotua new york hakuwahi hata kutembea states zingine aone utofauti.

na utuache siye tule starehe wewe endelea kula vumbi. hivi kwa nini nyie watu mlioko bongo mna wivu sana na siye tulioko majuu! na mtaendelea kutupapatikia kila tukija ovyooo!

Anonymous said...

Nina wasiwasi uliye comment hapo juu! Lazima utakuwa ni we mwenyewe mtu mzima ovyoo!

Anonymous said...

Anonymous 3 said...
"inchi yenu inaangamia nyinyi mko majuu mnachezeshwa ya moto haaaaaaaaaaa". hata Christopher Columbus aliacha Italy akaenda kutafuta maisha bora America. Le mutuz Malecela amerudi tanzania kwa sababu ni mvivu na hawezi kusapeti watoto na mke.








Anicetus said...

Anonymous 1: Sisi tunataka kucheza rhumba kwa hiyo tupelekeni sehemu ambayo tutacheza bila bughudha.
Kwa heshima yako, unachoomba utakipata.

Anonymous said...

Watu waliokosa viza za USA utawajua tu. Wanahasira sana sisi tuliopata. Kaeni tu huko mkigawana umaskini uliokithiri mkisubiri kujengewa barabara kwa msaada wa watu wa Marekani.

Anonymous said...

Anonymous 3:11pm kula tano,nimekupenda bure,kwanza kabisa maisha ni popote jamani whether in china,italy nk yote heri,nyie watu wa nyumbani mnaotuponda sie tunaoishi kwa Obama tuachezi tubebe mabox yetu,hatun'gatwi na mmbu,na tukienda hospital huduma zote tunazipata hata kama huna hela utatibiwa tu then utalipa polepole sasa nyie huko je???tuacheni tuburudike tunapopata burudani kama hizi mbona nyie huko kila siku mnaenda bar kunywa na kula nyama choma wakati sie tunabeba maboxi yetu?huyu le mutuz ni mvivu,kaja huju na meli kashukia N.Y. kaanza kuendesha matrucks and trailers yakamshinda na amekimbia child support,si ajabu anatamani sana kurudi but too late

Anonymous said...

ukumbi mzuri kweli unapendeza kingilio bei ghani?

Anonymous said...

Huyu atakuwa lemutuzi anahasira na watu America sijui wamemfanya nini kama vile kachanganyikiwa,ajinyonge basi ,zee nzima kazi kufatilia mambo ya uku ,mzee yatakushinda ,acha kulia kama mtoto wa mbuzi ,pole zako.

Anonymous said...

chezeni tu ya motoo,mduwara pia

na mjipooze na stress za huko kwenu.

cha muhimu muwambiye wakuu wenu

wa ccm wanavyokuja huko;mbona

wanakufanyeni watoto na

kukudanganyeni na issue ya uraia

pacha? mbona mpala leo

hawajaipitisha na wala hawana nia

ya kuipitisha muswada huo.

kwanini wanakufanyeni watoto

wachangaa kwa kukudanganyeni na

badoo kila siku mnawaabudu na

kuwaramba nyayo zao wakija.

na le mutuz willima malecela hawezi kufa kwa mikazi yenu ya huko.Mtoto wa mshuwa yule hajazaliwa wala kulelewa kimazi chana.Alipofungua macho yake anapozaliwa tu anaziona pesa kwao na kuishi maisha ya raha si ya karaha.

kakuachiyeni nyinyi mikazi yenu ya kutokwa na roho na mistress ya kupiga boksi mnazo ziweza huko.
na afadhali wanakuja wamoto mzitoe mi stress yenu kwa kuserebuka.

halaaaaaa wapiga boksi wote wa marekani halaaaaaaaaaaaaa.

sisi tukija tunakuja huko na kurudi na biashara home hatukai tukafa kwa stress kama mlivyo huko.

mpango mzima wachina wanatujengea barabara si wamarekani mnao waabudu huko kwenu.

nendeni mkaserebuke na ya moto band huku nchi yenu inangamia nyinyi mmeshikila mistarehe isiyo na maana.faida ya kuwa huku nini badala ya kuwa na elimu na kujenga nchi yenu mnavaa vibwebwe na kuserebuka.

tutakutegemeeni nyinyi ndo dira na kioo chetu leo hii mnatu let down kwa mambo yenu ovyo ovyoo.

Anonymous said...

nani kakwambia weweeeee Tanzania ni maskini wangekuja hao wamarekani wako na wachina na wengi wengi kuja kuchota rasili mali zetu na kuja huko majuu kutibiwa hata akiumwa mtu ukuchaa.uongozi mbovu wa ccm ndo umetufikisha hapa tulipo na nyinyi huko ndo tegemo letu mnavishwa vibwaya na kuchezeshwa ngoma kama vinyamkeraaa.

tunakutegemeeni nyinyi mfanya ya maana mliopo huko majuu msinunuliwe na wana siasa na kulishwa propaganda za kizembe zembe.

tunakuombeyeni dua na kukutakiyeni maisha mema hatuna wivu na nyinyi kabisa.

na nyinyi mtuombee dua wote tunahitajiana hakuna aliye bora.

Anonymous said...

wewe anony wa March 10, 2015 at 3:46 PM
kwani utu uzima ni ugonjwa? wewe ndo ovyooo squared

Anonymous said...

mimi sielewi tatizo liko wapi watu wakila starehe zao tena kwa gharama zao wenyewe. sidhani kama hako ka $100 kanaweza badilisha nchi iliyooza kama Tanzania

Anonymous said...

Acheni roho mbaya. Kila mtu kaja kwa njia zake. WESTERN UNION na MONEYGRAM wafunge ofisi zao huko tuone matokeo. Msitudharau tumechangia sana maendeleo ya nchi. Tupendane wote wa bara la Africa. Haijalishi unaishi Artic , Africa kusini, Uchina, Geneva. Wote shina letu moja AFRICA.

Anonymous said...

Du mtu abebe boksi asibebe wewe unataka nini,.hayakuhusu,

Anonymous said...

Hivi hawa wabongo ambao wanakula vumbi huko na maisha yaliwashinda USA wanafikiri kila MTU aliyekuja USA ni mbeba box?. Mbona watu tuna life nzuri huku USA na tuna miradi ya maana bongo. Watu tuna paper na elimu na business vile vile. Bongo yenyewe nimeenda huko juzi juzi vumbi tupu. Wachache ndio wenye pesa ...niache kufanya issue zangu za msingi za kimaisha huku eti nikakimbizane na CCM bongo. Watu tupo USA na tumetoka vile vile. Sio kila MTU aliyekuja nchi hii Kaja na mchango wa wanakijiji jamani. Njooni USA mtembee state zote muone watu tulivyopiga hatua..msilinganishe hao wabongo ambao walikuja huku bila dira mkadhani kila mtu Hana dira huku. Eti lemutuz mtoto wa mshua..kitu zima limekimbia..familia..huku..please wabongo sio mnaona wivu tuu kwa kukwama kimaisha huko bongo...ni shiidah aisee..

Anonymous said...

Wabongo wa bongo acheni zenu kutufatafata starehe garama na tunazigaramia sio nyinyi mnazipingia mbizi mnapenda bure kila kitu.tuki jamba huku nyinyi mshavuta pumziiiiii duuu find something to do wabongo vumbi.

Ny Ebra! said...

Kelele za chura aziwezi kusababisha Tembo kuto kunywa maji. Save your date and come enjoy with us maisha ukiwa happy ata siku ya kufa unakufa na smile yako usoni kiroho safi.

Anonymous said...

Hahahahahahahah! Unakufa na smile! Marekani raha! Acha wala vumbi watuonee wivu

Anonymous said...

chezea vumbi...ukikohoa vumbi, ukipenga vumbi, maji ya kuoga yenyewe ya kuhesabu, hapo utashindwa ku-data kweli! jamani tukutane pale kwa raha zetu...

Anonymous said...

nendeni mkajiburudishe na mi stress yenu na mibaridi yenu.eti bongo kuna vumbi baki huko huko na usije.unaka huko hata kama una makaratasi yako but huheshimiwi.kwani unadhani hatuoni wanavyopigwa wazawa weusi na mapolisi mtakuwa nyinyi wadanganyika.

Anonymous said...


Kumsapoti anonymous wa march 13, 2015-1:45 PM : watanzania wote wa ugaibuni kutoka kwenye ngazi zote wanaombwa wakutane mahali hapo ili tuonyeshe mfano mzuri kama tunaweza kufanya mambo ya maendeleo na kuchangia uchumi wa nchi kwa kuongeza utalli nchini Tanzania pamoja nakuimarisha uhusiano wa Wamerikani na Tanzania- promoting Tanzania Tourism and Cultural Exchange
Hii ni project ya watanzania wote walioko ugaibuni na watanzania walioko Bongo.

Anonymous said...

Mbona bongo polisi wanacharanga watu hata hadi ktk maandamano ya sasa. Kwani baridi kitu gani. Wabongo kwa ushamba mbona ni season tu tena inapendwa. Nyingi huko joto mmekuwa weusi Kama mkaa..mmechoooka..wivu tu hamkupewa visa..mbona tupo huku hatujauawa na polisi sasa..tafuta point ya maana sio huh wivu wako usio na mantik kijana..USA oyeaah!

Anonymous said...

JAMANI KIASI GHANI KIINGILIO TUJUZUINI PLEASE MIMI NATAKA NIJE NISEREBUKE HASAAA MAMBO YAKUISAIDI NCHI YANGU NIMESHAACHANA NAYO NI MMAREKAI SASA NA HAPA NIMEKUJA KUPIGA BOKSI LANGU NA KULA RAHA.

SHUKRAN SANA KWA WALE WOTE WALIOFANIKISHA KUWALETA YAMOTO.

TUJUZUNI KIINGILIO KIASI GANI TUJE TUSEREBUKE SNOW IMESHAKWISHA SASA KULA RAHA NA BATA KWENDA MBELE KWA MBELE NA MWENDO WA MDUNGO.

WABONGO HUKO HOMU TUSIKILIZIENI SISI KWENYE MITANDAONI NDO TUMESAFIKA SUNATESA KINONA NONA NA MABOKSI YETU.

VIJIMAMBO OYEEEEEEEEEEEEEEE.RAHA TUUPU NY YAMOTO YA MOTO YAMOTO WANAPUUZA NA JOTO KWENYE HII SNOW..

Anonymous said...

Wewe unaesema hatuheshimiwi huku marekani wewe nani anaekuheshimu huku bongo???viongozi wenu wanawaibia kila kukikucha huko ni kuheshimiana gani huku,viongozi wenu wamekula mahela kibao ya Escrow nyie endeleeni kulala tu,sisi tumekuja kutafuta madola yetu huku hatuhitaji kuheshimiwa,tunakula bata tu na kubeba mabox kwa raha zetu