ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 15, 2015

TRAFIKI DAR WAENDESHA ZOEZI LA KUKAMATA BODABODA ZISIZOFUATA SHERIA

Askari wa Usalama Barabarani wakiwa wamezikamata baadhi ya pikipiki ambazo madereva wake wamekutwa na makosa mbalimbali eneo la Mbagala Rangi Tatu asubuhi hii, ambapo walilazimika kulipa faini ya shilingi 30,000/=
Askari wa Usalama Barabarani wakiendelea na ukaguzi wa bodaboda.
Vijana wakipandisha bodaboda ndani ya gari tayari kwa kuzipeleka Kituo cha Polisi Maturubai kilichopo Mbagala Kizuiani, Dar.
Askari Polisi wa Usalama Barabarani wakisimamia upandishwaji wa bodaboda hizo kwenye gari tayari kwa kupelekwa kituo cha polisi.

Askari wa Usalama Barabarani wa jijini Dar-es-Salaam wameanzisha msako wa kukamata bodaboda zinazokiuka sheria barabarani kama kutovaa kofia ngumu (helmenti), kupandisha abiria kwa mtindo wa mshikaki, kutokuwa na leseni za udereva na ubovu wa pikipiki hizo, lengo likiwa ni kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na majeruhi.

(STORI/HABARI: KULWA MWAIBALE WA GPL)

No comments: