Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akiongoza kikao cha Ujumbe wa Tanzania unahodhuria mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya wanawake unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kila asubuji wajumbe hukutana na kuhabarishana taarifa za mikutano waliyohudhuria siku iliyotangulia na kisha kupangiana majukumu ya siku hiyo. Ujumbe huu unashirikisha washiriki kutoka Tanzania Bara na Visiwa.2. Katibu Mkuu kutoka Serikali ya Mapunduzi Zanzibar Bi. Asha Ali Abdullah akifuatilia majadiliano kuhusu wajibu wa wanaume na wanavulana katika kufikia usawa wa kijinsia
Katibu Mkuu Bi. Anna Maembe naya akifuatilia majadiliano kuhusu wajibu wa wanaume na wavulana katika kufikia usawa wa kijinsia
Katika picha hii wanaoneka Mawaziri Mhe. Zainabu Omar Mohammed, kutoka Serikali ya Mapunduzi Zanzibar na Mhe Sophia Simba kutoka Serikali ya Muungano wakiwa na mwenyeji wao Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Balozi Tuvako Manongi akizungumza katika moja ya mikutano ya pembezoni ya Kamisheni kuhusu dhadi ya wanawake. Balozi Manongi alikuwa mmoja wa wazungumzaji walioalikwa kuzungumzia uwezeshaji wa wanawake kwa kupitia vyanzo mbalimbali kama vile mifuko ya maendeleo na mitaji mingineyo ili waweze kujitegemea kwa katika kumiliki mitaji ya kiuchumi kama sehemu moja wapo ya kuondokana na umasikini. wazungumzaji wengine katika mkutano huu kutoka kushoto ni Dr. K. Kellie Leitech, Waziri Ajira na Hadhi ya Wanawake kutoka Canada, Bi.Asa Reigner, Waziri wa Watoto, Wazee na Usawa wa Kijinsia kutoka Sweden ( watatu kutoka kushoto)
Wajumbe wakifuatilia majadiliano kuhusu uwezeshaji wa wanawake, ambazo wazungumzaji wakuu walikuwa ni Balozi Tuvako Manongi, Waziri K. Kellie kutoka Canada na Waziri Asa Regner kutoka Sweden katika mchango wake, Balozi Manongi alisema mifuko ya uwezeshaji ambayo imeanzishwa nchini Tanzania ni moja ya mafanikio ambayo imeweza kuwakwamua wanawake kuondokana na umaskini. Baadhi ya mifuko hiyo ni Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake kwa Tanzania Bara na Mfuko wa Maendeleo ya wanawake wajasiriamali Tanzania Visiwani.pia alielezea miradi mbalimbali ya uwezeshaji wa wanawake ambayo inafadhiliwa na wadau wa maendeleo kama vile Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji ya Umoja wa Mataifa ( UNCDF) unaofadhili mradi wa kuzalisha umeme huko Mkoani Iringa. Majadiliano hayo yaliandaliwa kwa ubia wa UN- Women, UNCFD na UNDP
Na Mwandishi Maalum,
New York
Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu
Hadhi ya Wanawake ( CSW) umeingia wiki
ya pili ambapo wajumbe wameendelea kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mada mbalimbali zinazohusu
hadhi ya mwanamke na mtoto wa kike.
Jana Jumatatu miongoni mwa majadiliano ambayo yamevutia wajumbe wengi
yalihusu wajibu wa wanaume na wavulana katika kufikia usawa wa kijinsia.
Katika majadiliano hayo
ilielezwa kwamba ili kufikia usawa wa kijinsia,
basi hapana budi kuhakikisha kwamba wanaume na wanavulana
wanashirikishwa kikamilifu katika safari
hiyo.
Imeelezwa katika majadilianao hayo kuwa Ushiriki wa
wanaume na wavulana kutaongeza kasi ya
kufikiwa kwa usawa wa kijinsia, na kwamba
jukumu hilo haliwezi likawa la wanawake
peke yao.
Baadhi ya nchi zilichangia uzoefu wao wa namna gani zinatekeleza
dhana hiyo ya kuhakikisha kwamba wanaume na wavulana
wanatimiza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba jamii
yote inakuwa na uelewa na ushiriki sawa katika kufikia lengo la kuwa na usawa wa jinsia.
Pamoja na majadiliano kuhusu mada hiyo, wajumbe
wanaoshiriki mkutano huu pia wameendelea
na majadiliano ya mada nyingine nyingi zilizokuwa zinafanyika katika
kumbi mbalimbali za mikutano hapa Umoja wa Mataifa
Baadhi ya mada hizo ni ile iliyohusu : kubadlisha
kanuni za jamii, ili kufikia usawa wa
kijinsia, matarajio na fursa.
Ajenda kuu ya Mkutano
wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi
ya wanawake, unaohudhuriwa na wajumbe
kutoka nchi wanachama wa Umoja wa
Mataifa, Taasisi za UM na wawakilishi kutoka Asasi Zisizo za Kiserikali,
ni Azimio la Beijing na Jukwaa la utekelezaji, miaka 20 baada ya kufanyika mkutano wa nne wa kihistoria wa wanawake, mkutano
uliofanyika mwaka 1995 Beijing, China.
Kupia Ajenda hiyo ya Beijing+20) wajumbe wanajadili changamoto za utekelezaji wake na mafanikio
katika usawa wa kijinsia na
uwezeshaji wa wanawake.
Wajumbe pia wanajadili matokeo ya kikao maalum
cha 23 cha Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, tathmini ya miaka mitano baada
ya kupitishwa kwa jukwa la utekelezaji, tathmini iliyoainisha hatua Zaidi na
mipango inayotakiwa kutekelezwa ili kufika
lengo la usawa wa kijinsia na uwezeshaji.
Vile vile mkutano
huu unajadili fursa kwaajili ya kufikia
usawa wa kijinsia na uwezeshaji kupitia ajenda mpya za maendeleo baada ya
2015.
No comments:
Post a Comment